ILIKUA HIVI, SASA IKO HIVI.

Kuna wakati mtu anaweza kufanya kitu halafu ukajiskia kama vile amekutenda vibaya… Wachana na maswala ya kimwili na kifeelings… Najaribu kukuzungumzisha kuhusu maamuzi flani ya serikali yanayofanywa kwa kisingizio cha maendeleo. Kwani we unataka maendeleo kweli?

Mfano Mwaka nimeperuzi mtandaoni hapa sasa hivi. Keyword Serikali yakataza mifuko ya plastiki. Moja kati ys tori zilizotokea ni ile mwaka 2013 ambapo serikali ilianza mchakato wa kuzuia matumizi ya mifuko hii hatari kwa mazingira. So back in the days I mean 2013 wakati wa uongozi wa Rais Kikwete Waziri aliyekuwa na dhamana ambayo Mh January Makamba anayo hivi sasa Mh Dr Tereza Uvisya Waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira (Wakati huo) Alikuwa ndio msimamizi wa ukatazaji wa matumizi hayo. Moja kati ya challenges zilizotokea miaka hivyo ni kwamba.

Serikali ilitumia mbinu complicated kidogo kukataza matumizi ya mifuko ya Plastiki, maana kulikuwa na katazo la mifuko ya unene wa maikroni 30… (Hivyo ilikuwa ni kazi ya muuzaji kuhakikisha dukani kwake hana mifuko ya maikroni hizo, Je atafahamu vipi mifuko hiyo? Lilikuwa swali gumu na majibu mengi ya kisiasa na kisayansi) Hatua ya wananchi kuitambua mifuko iliyokatazwa ikawa ngumu sana. Baadae serikali ikahamisha katazo kwenye mifuko ya Maikroni 100. Wakati wote huu ukumbuke watu wanahitaji huduma na hawana vifungashio mbadala ambavyo serikali iliviweka tayari… na pia wananchi hawa hawana uwezowa kutambua tofauti ya Maikroni wala nini. Zoezi hili baadae likawa limefeli. Na hivyo ndivyo ilikuwa mara ya mwisho katika harakati za kuokoa mazingira kutokana na plastiki hizi ambazo hukaa kwenye ardhi kwa muda mrefu na kusababisha athari kubwa.

Pangáng;a mingi juu ya mifuko hii na athari zake ziko kwenye mtandao (TAFUTA MUDA UPITIE) Cha msingi sana hii leo ni kutambua kuwa jiwe linaweza kuwa jiwe siku zote za maisha yake, lakin tabia na utendaji wa serikali hauwezi kufanana wakati wote. Mwaka 2015 Baada ya Tanzania Ku Upgrade uongozi wake Makamba akapewa dhamana ya Ofisi ya mazingira. Kulikuwa na makando kando kibao katika ofisi hii na mojawapo ni hili ambalo lilimshinda Mh waziri wa wakati huo chini ya uongozi wa Jakaya. Je chini ya Makamba na Magufuli litawezekana? Mpaka sasa tunaona Uproach tofauti kidogo. Mwaka 2016 Millard Ayyo alipost video ya Waziri Makamba na tamko lake rasmi kuwa ifikapo 2017 utakuwa ni mwisho wa kutumika mifuko hii ya plastiki… Mimi mwenyewe nikajua mkombozi amekuja kwa wajasiriamali ambo wanatafuta fursa wangeingia kwenye uzalishaji wa mifuko ya karatasi ili kureplace hii ya plastiki.

Leo ndio umefika ule muda alioutangaza waziri makamba na viroba vimepigwa marufuku. Hii ni changamoto mpya kabisaaa maana wale ambao walikuwa wanauza na kutengeneza pato lao la kila siku kwenye viroba hawawezi kufanya hivyo sharia itamfyagia mtu… Na wale ambao walikuwa wanapiga starter kwanza kabla ya kuanza siku asubuhi hawawezi tena… Kiroba na Bangi selo ni ile ile moja. Bado nauliza Kwa uongozi wa Makamba hili litawezekana?

Mimi naona hapa malalamiko yaendlee tu ila serikali imechukua pointi tatu muhimu juu ya wahusika na wahanga wa kupiga starter… Hata kwa wauzaji. Kulikuwa na muda wa kutosha na serikali iliweka taarifa na muda ambao katazo rasmi litaanza kufanya kazi. Ni zaidi ya miezi nane imepita tangu taarifa zitolewe, kama ulikuwa hujaandaa mbinu mbadala ya kustua ndani ya miezi nane na bado hujajiandaa kuacha kuuza Viroba ndio basi tena. tangu ameingia madarakani Mh Magufuli tujue tu amekuwa akisema kitu anahakikisha anakitekeleza. 2013 ilikuwa hivi sasa 2017 hivi Iko hivi. Je kuna tatizo?

Endelea kufuatilia Watupipo.com kwa habari na sanaa. Cheki na team ya @watupipo.com Facebook na @watupipo.com Instagram.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com