JELA KWA KOSA LA KUMPA MIMBA MCHUMBA WAKE.

Sheria za kiislamu nchini Abu Dhabi zimepeleka majonzi makubwa nchini Afrika Kusini baada ya raia wa nchi hii ya Africa Emlyn Culverwell 29, kufungwa uarabuni kwa kosa la kumpa ujauzito mchumba wake Iryna Nohai, 27 raia wa Ukraine. “usishangae”

Tukio hili la kutia hasira limewakumba wapendanao hawa January 29 siku mbili tu baada ya kufunga uchumba. Baba mzazi wa Emlyn amesema kwamba wawili hao walifunga uchumba huo baada ya kugundua kwamba Iryna ni mjamzito.

Siku ya tukio wawili hao walifika katika kituo cha afya baada ya Iryna kupata maumivu ya tumbo, daktari alipogundua kuwa ni mjamzito akaulizia cheti cha ndoa ambacho hawakuwa nacho… ndipo daktari akapiga simu na kuripoti polisi mara tu alipogundua kwamba ni mjamzito.

Baba mzazi wa Emlyn alifikishwa hospitali mara tu aliposikia habari hizo mbaya, lakini baadaye alipata nafuu. “Nilikuwa nasubiria kwa hamu sana kumuona mkwe wangu maana kwa jinsi nilivyoona kwenye picha anaonekan ni msichana mwema sana” alisema Mr Culverwell.

Kuna confusion kibao kwenye hii stori lakini cha msingi ni kwa couple mnaosafiri Arabuni mkae chonjo… Sheria za kiislamu zinasema kwamba Iryna anakabiliwa na mashtaka ya “Zina”ambayo hukumu yake ni kifungo jela. Japokuwa takribani wiki sita tangu wakamatwe bado hawajashitakiwa huku taarifa zikisema kuwa mamlaka zinafanya vipimo zaidi.

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com