JAGUAR, KUTOKA DRUGS KUELEKEA BUNGENI

Rumours zilianza kutawala tangu alipoteuliwa na rais Uhuru Kenyata kuwa Director wa Mamlaka ya kupiga vita ulevi na madawa ya kulevya nchini Kenya NACADA mwaka 2015. Baadhi walianza kuona kuwa msanii Jaguar ameanza kujiingiza au kupewa nafasi ya kuwania seat kubwa zaidi kwenye uwanja wa politics za Kenya.

January 2017 Jaguar aliandika barua ya kuachia ngazi ya kuongoza mamlaka hayo kwa kusema kuwa ana sababu zake binafsi ambazo zilikuwa obvious kwa wachambuzi wa siasa mitaa ya Nairobi.

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa miaka miwili ambayo mkali huyu wa Kigeugeu amekuwa akihudumu kama Director wa mamlaka haya amekuwa akifanya kazi nyingi na vijana hasa maeneo ya Slums aka uswahilini, kazi hizi zikiwa ni pamoja na charity works kitu ambacho baadhi wameona kuwa ni mafanikio kwake na anastahili kupongezwa. “Kama kijana ametimiza kile ambacho ametakiwa kukitimiza kwa vijana wenzake” amesema mmoja wa wapenzi wa muziki wa Jaguar alipokuwa akiongea na Watupipo.com na kuongeza “vijana wanahitaji inspirations kutoka kwa watu kama Jaguar ili kuacha madawa ya kulevya na ulevi”

 

 

 

 

 

 

 

 

Habari zimetapakaa kila kona ya Nairobi sasa ni kuwa msanii huyu ambaye pia amefanikiwa katika entrepreneurship, anatarajia kuingia vizuri sasa kwenye siasa kwa kugombea kiti cha “Starehe Nairobi MP” ambacho ataingia akiwa na jina kubwa katika muziki na kazi nyingi za kijamii alizofanya kurahisisha au kubadilisha maisha ya watu wa chini.

Jaguar anaingia kwenye list ya wasanii wakubwa wa Hip Hop ukanda wa Africa mashariki kama vile Prefessa Jay wa Tanzania ambaye mwaka 2015 alichaguliwa kuwa MP, Boby Wine wa Uganda ambaye aligombea kiti cha MP na Mr II aka Sugu ambaye ni MP wa Mbeya tangu mwaka 2010 na wengine wengi.

Watupipo inamtakia Jaguar safari njema na nguvu ya kuendelea kuhudumia vijana wenzake kwa nafasi aliyonayo kwa namna yoyote ile anayoweza.

Photo credits: Msetoea, mwakilishi.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com