BANGI INAWEZA KUKUPA UGONJWA WA MOYO – TAFITI

 

 

 

 

 

 

Tafiti mpya imefanyika na kuonesha kwamba matumizi ya bangi “marijuana” yanaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Hii nimeidaka kutoka kwenye taarifa iliyotolewa na shirika la CBS News.

Taarifa zinasema kuwa Dr. Aditi Kalla kutoka Philadelphia Einstain Mediacal Centre alifanya utafiti huo kwa kutumia rekodi za wagonjwa milioni 20 na kugundua kuwa kati ya hao asilimia 1.5 walikubali kuwa wanavuta “bangi” na ikaonekana bangi inaweza kuchangia asilimia 26 ya hatari kupata ugonjwa wa moyo. “keyword; inaweza”

Pengine haya maasilimia yanaweza kukuchanganya, Botom line is, japokuwa bangi ina raha zake na inazo faida zake kibao bado kunazo hasara zake pia ambazo nyingine zimethibitishwa na nyingine bado ni “myth tu” so nimeona nikuorodheshee baadhi ya faida na hasara hapa ili kabla hujawasha “chombo” ujue kabisa kipi ni kipi.

 

 

 

 

 

 

 

 

  1. Imedhihirika kwamba bangi ina faida kwa wagonjwa wa cancer kupunguza maumivu, pia inaongeza Congnitive functions (attention, reasoning, memory) pia bangi inachangia katika matibabu ya cervical cancer, pamoja na faida zingine nyingi ambazo hazijafanyiwa utafiti.

2. Lakini kwa upande mwingine kabla hujawasha nyingine, ni vizuri ukifahamu kwamba kwa kuwa msuba unaathiri cognitive functions imedhihirika kwamba zipo athari katika kumbukumbu za muda mfupi, pia unaweza kuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa mifupa “Osteoporosis” kama ukiwa mvutaji wa hali ya juu. Zipo pia athari zingine ambazo bado hazijafanyiwa utafiti.

Pamoja na kwamba bangi imekuwa debate kubwa na baadhi ya nchi zimekwenda mbali zaidi na kuhalalisha matumizi yake, ni maamuzi ya mtu binafsi kuchagua kuvuta au kuvuta. Ni afadhali usipovuta kabisa kama bado hujajaribu na kuona utamu wake lakini kama unatumia tu kwa nia njema na inakupa faida kadhaa basi na uendelee tu, hakikisha unafanya siri kwa sababu uvutaji wa bangi sio kitu cha kujivunia.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com