KATI YA BIASHARA TANO ZA AJABU. IKO YA KUKUMBATIANA.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

NO 5: KUKUMBATIANA

Kampuni ya Cuddle party imeanzishwa mwaka 2014 na biashara kubwa wanayoifanya ni kusababisha Party ambayo watu hukutana na kukumbatiana. Unapokuwa kwenye party hii ambayo watu tofauti wasiofahamiana hukutana, unaweza kumu-aproach mtu yeyote na kumsalimia na kisha kumuomba kumbato lake. BASI

Najua baadhi ya mafisi wanaweza kuona kwamba hii ndio party wanayotakiwa kwenda NO! Kwenye party hii ya kukumbatiana kampuni hii imeainisha malengo makuu ya kufanya party hii ni kwa watu wazima ku-explore Mapendo, maridhio pamoja  na mawasiliano. Katika usajili kampuni hii ni NGO ya elimu.

NO 4: MESSAGE ZA VIAZI

Unaweza kucheka lakini biashara ya kutuma ujumbe kwa kutumia viazi inafanyika na watu wanatengeneza mkwanja. Kwa mujibu wa site ya Potato percel huduma zao zinatarget watu wanaotaka kutuma fun message kwa mtu lakini hawafahamu watatumaje.

Unachotakiwa kufanya ni kuandika ujumbe wako usiozidi maneno 15, nakisha unautuma kwao. Ni hivyo tu mlengwa wako atapelekewa ujumbe ukiwa umeandikwa juu ya kiazi… Ndugu zangu Wapare “kiogwe” au kwa wakikuyu “waruu” ukitumiwa message kwa njia ya kiazi tayari unashukuru kwa kupunguziwa budget ya hiyo siku. Kampuni hii haitatuma ujumbe wowote wa chuki au matusi.

NO 3: WAFUNGISHA HARUSI WANAOTEMBEA.

Well mpaka sasa umeshawahi kushuhudia nap engine kutumia huduma za chakula kwenye gari maalumu linalozungusha huduma zake mjini, au pengine umeshapata Ice cream kutoka kwa baiskeli maalum mtaani, Lakini nina hakika hujawahi kufunga ndoa kwenye gari maalumu linalozungusha huduma hiyo mtaani.

Wedding Chapel, ni huduma ambayo inakurahisishia hustle zote za kuandaa mazingira ya kufunga ndoa kwa $125 pekee. Unachotakiwa kufanya ni kupiga simu na kusema mnataka kuoana na muda sio mrefu watafikisha huduma hiyo pale ulipo. Huduma hii inakuja na mfungishaji ndoa, mashahidi, na wakati mwingine wanakusaidia kupata eneo zuri la kufungia harusi yako kwa gharama nafuu. Haya wale wenzangu na mie ambao hamuoi kwa kukwepa gharama hii inawahusu.

Je unadhani hii biashara inaweza kufanikiwa maeneo ya kwenu?

 

 

 

 

 

 

 

NO 2: RECYCLE BOXES

Mara kadhaa umekuwa unahitaji boxes kwa ajili ya kuhifadhi vitu au kuhama nyumba, Iwe sababu yoyote ile kuna kampuni ambayo iko maalumu kabisa kwa ajili ya kukuuzia boxi na kama ukimaliza kazi na huna pa kulipeleka unaweza kuwauzia tena kwa ajili ya mteja mwingine. Biashara hii inaweza kufanyika hata hapa nchini maana mara kadhaa watu wamekuwa wakihitaji Boxes na wakati mwingine huwaga vigumu kupata box ambalo litakidhi mahitaji yako.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

NO 1: RAFIKI ANAYENUKA

Umeshawahi kuwa na rafiki ambaye anatoa harufu mbaya mpaka unajiskia aibu mbele za watu as If wewe ndio unanuka? Basi SWAGO SCENTS, wanatoa huduma ya kutuma ujumbe kwa rafiki kama huyo bila yay eye kujua ni nani amemwambia kuwa ananuka. Kampuni hiyo ambayo pia inauza bidhaa za manukato inakupa nafasi ya kumsaidia rafiki yako na kupitia website yao unaweza kutuma ujumbe na wao watahakikisha wanampelekea Scent wipe ikiwa na note ambayo inaonesha rafiki yake amemjulisha kwamba swala la kunuka sasa ni MWIKO!

Kampuni hiyo imehakikisha kwamba hakuna namna yoyote ambayo rafiki huyo anaweza kujua kuwa wewe ndio umemtumia ujumbe na bidhaa hizo za manukato labda uamue kufungua domo lako kumwambia. Hata hivyo unatakiwa kulipia $1.9 ili kumtumia percel hiyo inayoweza kubadilisha maisha yake kuanzia siku hiyo.

 

Kama kuna biashara nyingine unaifahamu ambayo ni ya ajabu please nistue niicheki pia kupitia Comment hapa. Otherwise asante kuitembelea http://www.watupipo.com/ na karibu tena.

 

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com