MICHEZO 5 YA WATOTO AMBAYO IMEPOTEZA UMAARUFU MIAKA YA SASA.

5. KOMBOLELA (Mchezo wa kujificha)

Moja kati ya michezo maarufu sana ambayo kila kundi la watoto wa karne iliyopita walikuwa hawakosi kuicheza. Mchezo huu una majina tofauti kutokana na jamii mliyokulia. Kwetu tuliita Kombolela kingereza wanaita “hide and seek” wengine nchini Kenya walikuwa wakiita brikicho

Mchezo huu ni mzuri lakini hatari pekee ilikuwa ni kwa wale ambao walikuwa wakicheza usiku, maeneo mengine ambayo yalikuwa na giza na kuna mmoja kati ya rafiki zangu aliwahi kugongwa na nyoka. Pamoja na hayo baadhi ya watoto watukutu walitumia mbinu ya kujificha ili wafanye “matusi”

 

 

 

 

 

 

 

4. KUENDESHA TAIRI

Huu mchezo miaka ya siku hizi haujaisha kabisa umaarufu katika jamii zetu, lakini ni kwa nadra sana utakutana na watoto wakicheza na matairi ya gari kama ilivyokuwa miaka ya zamani. Mchezo huu mimi binafsi umenipatia makovu mengi na nimepigana vita sana na watoto wengine kwa sababu ya kugombea matairi.

Moja kati ya sababu ambazo mchezo huu umetoweka ni pamoja na mazingira hatarishi ambayo yako maeneo mbali mbali na kwenye barabara zetu hivi sasa. Magari yamekuwa mengi na madereva wabovu ni wengi hivyo ni vigumu kwa mzazi kumuacha mtoto wake aende kukimbizana na tairi wakati anaweza kugongwa na gari anytime.

NO 3: KULA MBAKISHIE BABA

Mchezo huu ulikuwa unachezwa na kundi la watoto, Mchanga unakusanywa halafu juu ya kilele cha mchanga kunachomekwa kijiti na kwa pamoja watoto wanaanza kutoa mchanga kidogo kidogo kutokea pembeni. Masharti ya huu mchezo ni kwamba yule atakayeondoa mchanga na kusababisha kile kijiti kianguke anachapwa kama mwizi na kichapo kitaisha pindi tu atakaposhika au kufika katika eneo ambalo mmekubaliana.

Mara nyingi maeneo ambayo mtu anatakiwa kushika yalikuwa umbali wa kuanzia mita 20 na kuendelea. Japokuwa ulikuwa ni mchezo wa kufurahisha na wenye hatari kidogo ndani yake ulikuwa unafundisha ujasiri kwa watoto kwa sababu kila aliyekuwa anacheza mchezo huu alifahamu kwamba akidondosha kijiti anapigwa kama ameiba… na bado hiyo ndio ilikuwa burudani.

 

 

 

 

 

 

 

 

NO 2: TOBO MANGUMI.

Mpira wa miguu ni moja kat ya michezo maarufu sana kwa watoto mpaka leo hii, Lakini mpira ambao ulihusisha kuchapana fimbo mateke na mangumi umepotea miongoni mwa watoto. Kulikuwa na ina mbili za michezo ya mpira. Moja ambayo haikuwa maarufu sana ni ile ambayo kundi la watoto wanarusha mpira na kila anayeugusa anatakiwa kupigwa teke “butua” uzuri wa mchezo huu ni kwamba utaigwa teke pale tu unapokuwa na mpira mguuni kwako so mara nyingi unaweza usipigwe.

Mchezo ambao ulikuwa maarufu zaidi tuliuita “Tobo” kama ilivyokuwa kwa mcheo wa kula mbakishie baba, hapa pia kulikuwa na sehemu maalumu ambayo mtu anayekimbizwa anatakiwa kushika. Na ili uanze kupigwa kama umeiba unatakiwa mpira upitishwe kati kati ya miguu yako… Hapo utashambulishwa mpaka ukashike kwenye eneo ambalo mmekubaliana.

NO 1: MSINGI BOMOA

Ipo michezo mingine ambayo watoto walikuwa wakicheza na sasa hivi huwezi kuiona tena. Huu ni mmoja wapo. Mchezo huu ulikuwa hatari sana na sina tatizo kama watoto hawautaki tena.

Kilichokuwa kinatokea ni watu wawili mnapinga kwamba ukimkuta mwanzako ameinama au kuchuchumaa basi unampiga teke la makalio. Mara kadhaa mchezo huu umesababisha watoto kupigana kuumizana na mra nyingine kuunguzana na moto au kuangushana kwenye vitu vyenye ncha kali.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com