JINSI YA KUSTUKIA NEWS FEKI MTANDAONI

Story imebreak leo March 14, baada ya Mkurugenzi wa shirika la utangazaji Tanzania TBC Ayoub Rioba kuwafukuza watangazaji pamoja na wafanyakazi wengine 9 wa habari kutoka katika shirika hilo, baada ya kuingizwa mkenge na kutangaza habari za uongo kwamba rais wa Marekani amemsifia rais wa Tanzania kwa uchapaji kazi wake. “Hivyo tu ugali umewachoropoka”

 

 

 

 

 

 

 

Watupipo.com imekuchujia hizi mbinu chache za kugundua kwamba habari unayoisoma sio ya kweli. Ikiwa umepata habari hiyo kutoka mtandaoni vitu hivi ni vya muhimu sana kuangalia kabla ya kujiaminisha kwamba hiyo ni habari ya ukweli au sio.

  1. Mtandao ulioandika/ Chombo husika

Inategemea na habari yenyewe inahusu nini, ipo mitandao na mashirika ya kuaminika ambayo yanajulikana. Kuanzia TV Networks au magazeti ambayo yanaaminika kuwa mfano ITV, CLOUDS TV, KTN, CITIZEN kwa TV za Afrika mashariki pamoja na mengine, magazeti mfano The Guardian, The Citizen, Nation, na mengine ambayo kazi yao kubwa ni kutoa habari… Sasa ukuniuliza vipi kuhusu TBC? Jibu lake ni kwamba wamejishushia sana hadhi ya kuwa shirika la kuaminika pamoja n kufukuzwa kwa wafanyakazi waliotoa habari hiyo fake.

  1. Ukubwa wa habari.

Jiulize habari hii kwa ukubwa wake imeandikwa na mshirika mangapi? Kwa kawaida habari ikiwa kubwa huwa inaripotiwa na mtandao zaidi ya mmoja tena wa kuaminika.

 

 

 

 

 

 

3. Ueledi katika wa muandishi.

One of my Colleague ambaye ni producer mzuri sana wa Movie ameniambia yeye huwa anaangalia sana professionalism na jinsi stori ilivyoandikwa. Ikiwa hamfahamu mwandishi aliyeandika hiyo news basi ataangalia jinsi habari ilivyoandikwa. Lugha iliyotumika, spelling mistakes gramma na vingine vyote vinavyoiweka story machoni.

Kilichowakuta watangazaji wa shirika la TBC ni sawa sawa maana wamechukua habari kutoka kwenye mtandao ambao hauaminiki na kuziweka kwenye News Bulletin ambayo inatazamwa na dunia nzima bila kuhakikisha kwamba ile habari ni ya kweli. Cha kusikitisha List ya waliofukuzwa kwa kuhusika ni wanataaluma ambao ni wasomi wa kujitosheleza na uzoefu wa kutosha kwenye media. Kulikuwa na sources kama BBC, CNN, the real FOX NEWS, na media nyingine kubwa ambazo kwa siku ile tayari zingeiripoti habari ya Donald Trump kumsifia Magufuli. Kuwa makini na fake news zinaweza kukuingiza matatizoni.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com