VIDEO: TUMEWEKEZA LAKINI WANGA NI WENGI – MAMONGÓO

Vijana kutoka Arusha maarufu kwa ngoma zao kama kimbaumbau, na digidigi wanaojulikana kama Mamongóo (vijana washamba) wamesema kuwa jamii ya sasa hivi inawatisha kutangaza mishe zao wanazofanya nje ya muziki.

Mamongoo wiki hii wakiwa katika ziara yao kikazi Dar es salaam, wamesema kuwa wao wanajihusisha na biashara nyingi ikiwemo kilimo na ufugaji kama zilivyo jamii nyingi mkoani Arusha. Lakini Mtangazaji  H2K wa Shujaaz radio show ya EA radio alipotaka kufahamu mishe zingine wanazofanya wasanii hao walisema hawawezi kumwaga mchele maana siku hizi wanga ni wengi.

“sisi pesa zetu hatujahifadhi benki ila tumeziweka sehemu ambayo tunajua zina mzunguko wa kuzalisha, na tumewekeza kwa vijana wenzetu” alisema chalii Jambo kutoka kundi hilo. Hata hivyo, walipoulizwa ikiwa kijana amepata pesa anatakiwa kuwekeza kwenye kitu gani kwanza kati ya shamba, nyumba au ardhi, walisema kwamba ardhi ndio kitu ambacho kinafaa kwa kijana kuwekeza kabla ya kununua gari au hata nyumba maana ardhi inaweza kuleta nyumba na gari.

Wasanii wengi siku hizi wamekuwa na kasumba ya kutumia mishe zao wanazofanya pembeni ya Sanaa sio kwa kujiongezea kipato pekee bali kujipatia heshima miongoni mwa fans wao. Mfano mzuri ni msanii Masanja Mkandamizaji ambaye kwa sasa amekuwa kutengeneza mamilioni ya pesa kutokana na biashara ya KilimoPesa, ambapo mara kadhaa kwenye Shujaaz radio show alimwambia Mtangazaji @DJTee255 kwamba kilimo ndio kinamlipa zaidi ya usanii.

Kipindi cha Shujaaz kinachoongozwa na mtangazaji machachari DJTee, kinaruka kila wiki kwenye radio tano nchini hivi sasa, East Africa Radio, Kings FM, TBC FM, Abood radio na Chuchu FM ya Zanzibar huku kikiwa ni kipindi pekee kinachokuja juu kikiwa kinahamasisha vijana kujiingiza katika ujasiriamali kwa fujo, ili kuweza kukuza uchumi wa nchi.

VIDEO: Mamongóo wakizungumza na H2K wa Shujaaz.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com