HII BURGER MOJA TU IMEENDA KWA $10,000 – DUBAI

Dubai katika mnada unaofanywa na kampuni ijulikanyo kama Pink Caravan zimeuzwa burger kadhaa na ya bei kali zaidi ilikuwa inakwenda kwa dola 10,000 tu. (TSh Mil 20 au Ksh Mil 2)… Kama umekuwa unapiga hesabu ni wapi utaamkia asubuhi kupata chai na chapati ya bei rahisi hasa msimu huu wa pesa chungu, amka haraka na ukatafute pesa unachelewa.

Aliyechukua mikate hiyo iliyowekwa nyama cheese na cheddar zee pamoja na veal bacon strips, ni mwanamama anayejulikana kwa jina la Asma Al Fahim ambaye ni founder wa magazine iitwayo Villa 88. Mkwanja ulioingizwa kwa kuuzwa burger 4 kwenye action hiyo ulikuwa ni zaidi ya Tsh milioni 50 au Ksh 5 Mil.

Bahati nzuri Mungu si Athumani, pesa za mnada huo zinapelekwa kuendesha kampeni ya cancer ya ziwa na pia kufanya vipimo vya kansa hiyo mapema. Good way to raise pesa Dubai hiyo hapo. BTW Burger hiyo ilikuwa na level saba, kitu ambacho Donald Trump na vimikono vyake vidogo hawezi kuishika.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com