JAMAA AMEUAWA BAADA YA KUMPORA ASKARI BUNDUKI – FRANCE

Leo hii March 18, asubuhi nchini Ufaransa Polisi wamemuua jamaa aliyejaribu kumpora Bunduki afisa wa jeshi, ndani ya uwanja wa ndege wa Orly. Mtu huyo ambaye jina lake halijawekwa bayana majira hayo hayo ya asubuhi katika eneo la ukaguzi wa polisi mjini humo alihusika kumpiga risasi polisi na kutokomea kabla ya kufanikiwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege.

Jamaa huyo baada ya kuingia uwanjani humo na kunyata mpaka kufanikiwa kumkaribia mwanajeshi mwanamke na kufanikiwa kumvamia na kumpora bunduki yake lakini kabla hajafanikiwa kuitumia silaha hiyo maofisa wengine wawili walimtungulia mbali na kufa hapo hapo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bruno Le Roux amesema mtu huyo amekuwa akifahamika na maofisa upelelezi na pia amewapongeza polisi waliofanikisha kumzuia jamaa huyo kabla ya kufanya maafa kwa kutumia silaha hiyo aliyopora. Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusisha tukio hili na ugaidi.

Ufaransa imekuwa moja katia ya nchi Ulaya zinazoshambuliwa mara kwa mara yakiwemo mashambulio ya kigaidi.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com