MC PILIPILI NA VIJANA WA TZ KUHUSU MADAKTARI WA TZ KWENDA KENYA – detail

Nimezungumza na vijana kadhaa, na kwa nyakati tofauti kusikia maoni yao kuhusu move ya serikali ya Tanzania kuruhusu madaktari 500 kwenda kufanya kazi nchini Kenya, kwa ajili ya kupunguza gape la upungufu wa madaktari, ulioonekana baada ya kutangazwa kuisha kwa mgomo wa madaktari wa Kenya ulidumu kwa zaidi ya siku 100.

Msanii maarufu MC Pilipili pamoja na Mtangazaji wa zamani wa luninga Allan Lucky ni miongoni mwa vijana waliozungumza na watupipo.com na kutoa maoni yao.

“Ni habari mpya ambayo ndio naisikia kutoka kwako, lakini kwa nionavyo mimi hakuna ubaya. In fact sisi kama wana Afrika Mashariki ni lazima tusaidiane inapohitajika” alisema Allan Lucky ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi jijini Nairobi. Kijana mwingine ambaye ni Mtanzania aishiye Nairobi Rabii Kinyogoli yeye alishangaa¬†baada ya kusikia habari hizi.

“Kwanza kabisa nina mixed reaction, maana kwa ninavyojua Tanzania wenyewe tunahitaji waganga hawa, sio kwamba wametosha. Pili ni kwamba huu mgomo ambao unafanyika sasa hivi je, ukiisha itakuwaje hao madaktari ambao wanakuja watarudi Tanzania au ndio wanakuwa wafanyakazi wa kudumu?” Alisema Mtanzania huyo ambaye amesoma na kufanya kazi jijini Nairobi kwa miaka kadhaa sasa.

Msanii wa ucheshi maarufu kwa jina la MC PiliPili yeye ameonesha kutounga mkono move hiyo ambayo imetangazwa leo, baada ya Rais wa Tanzania Dr Magufuli kutoa ruhusa hiyo baada ya kutumiwa maombi na Rais Kenyata. MC PiliPili yeye amesema kwamba ikiwa ziko pesa za kuwalipa madaktari watanzania, ni kwa vipi serikali ya Kenya isiwalipe madaktari wa Kenya ambao wanastahili zaidi kufaidi ajira za nchi hiyo?

Msikilize MC Pilipili hapa na yote aliyosema…

Mnamo mwaka 2012 ilichapishwa ripoti inayoonesha kuwa kuna upungufu mkubwa wa madaktari nchini Tanzania hasa kwa maeneo ya vijijini, kwa ratio ya 0.31 doctors kwa raia 10,000. Lakini pia tangu mwaka 2009, serikali ya Tanzania ilichukua hatua madhubuti kuwapeleka madaktari shule na kutrain wasaidizi mpaka kufikia level ya udaktari ili kupunguza tatizo la upungufu wamadaktari.

Lakini pamoja na kuongezeka kidogo kwa graduate miaka mitano baadaye serikali haikuwa na mipango madhubuti ya kuhakikisha madaktari hao wanapata ajira na hasa maeneo ya mikoani na vijijini. Hivyo lundo la madaktari waliohitimu wakabaki kuachana na fani hiyo kuingia kwenye fani zingine huku wengine wakiwa hawana cha kufanya kwa kukwepa mazingira magumu ya kufanya kazi vijijini.

Kauli ya rais imewaita wale wote ambao wamehitimu fani ya udaktari na kumaliza intenship kwenda kuhudumu nchini Kenya kwa kuwa bado serikali haijafanikiwa kuajiri madaktari wote, na sio kwamba Tanzania imeshamaliza tatizo la upungufu wa madaktari. Prediction iliyofanywa na National Center for Biotechnology Information ya Marekani imeonesha mpaka kufikia mwaka 2025 ratio ya madaktari Tanzania itaongezeka kufikia 1.04 kwa raia 10,000. NO SO BAD?

Kama wewe ni mpenda data cheki hizi hapa nimekukusanyia. Niwie radhi kwa maneno madogo

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com