NOMA : KUNA TEKNOLOJIA INAYOJUA UNACHOFIKIRIA KABLA HUJATAMKA

Kabla sijalala usiku wa leo tarehe 21 March, limenijia wazo “je mlango nimefunga? Baada ya kuhakikisha nikafikiria “hivi itakuwaje siku moja mtu akigundua kifaa ambacho kinamuwezesha kuona au kuingia katika nyumba yangu bila kutumia mlango” Je sayansi kama hiyo itakuwa ina faida au itakuwa noma.

Anyways nikaperua kwenye Google kutafuta “scary science inventions” … Katika lundo lote la majibu, nikavutiwa na stori ya mwanamama ajulikanaye kama Mary Lou Jepsen. Kabla sijakuelezea Mary ni nani, nikuambie kwamba kampuni yake anayoimiliki ya Opnwatr, inafanyia kazi technolojia ya MRI inayoweza kujua mawazo ya binadamu kabla hujafungua mdomo wako. Imagine wale walioko karibu na mzee Magufuli wangekuwa wanajiwazisha nini kuepusha utumbufu?

Jepsen, ni mwana-tech ambaye ameishi na kupumua tech kwa miaka kibao. Na sio tech zetu za kibongo za kurekebisha simu pale mtaa wa Congo, yeye ameshafanya kazi Facebook katika kitengo cha Facebook Oculus (hii ntakuelezea zaidi next time) lakini pia Jepsen amefanya kazi na kampuni ya Google kwenye kitengo chao cha sayansi cha Google X.

So hivi sasa anatuambia muda sio mrefu ndani ya miaka mitatu around hapo, kwenye technolojia hii mtu ataweza kukuweka kwenye MRI na akajua unachotaka kusema kabla hata hujatamka kitu, kama unamsikiliza au unamu-ignore, pia anaweza kujua ni ngoma gani unataka kuiskiliza sasa hivi. Moja kati ya vitu ambavyo vinawezekama kwa technolojia hii na ninaona ni vya maana zaidi… ni ishu ya kukifikiria kitu na kikatengenezeka kwa maana ya kwamba ukaunda kwa kuwaza PEKEE. Mfano ukiwaza kitu ambacho kinafaa kuundwa na 3D machine ina maana kingeprintiwa chap!

Lakini Jepsen kwa sababu ni mwanasayansi anajua hatari inayoisogelea dunia ikiwa gunduzi nyingi “deep” kama hizi zitaingia sokoni kabla ya kuwepo kwa sheria za Kudhibiti matumizi mabaya. kwa polisi pengine zitakuwa na faida na kwa baadhi ya watu lakini Magaidi wakiwa na vifaa kama hivi unadhani itakuwaje?

Amesema akili ya mwanadamu ni kitu chenye nguvu sana… Kinachoponza akili isifanye vitu kwa full power ya akili ni physical nature. Lakini wakati ambapo tutakuwa na Artificial inteligence na bots (roboti) zinazoweza kuatenda kwa ufasaha na haraka mithili ya akili zetu zinavyowaza, sitaki kuwaza yale ambayo yangekuwa yanatendeka. Endelea kutembelea watupipo.com mara kwa mara nitakuwa nazungumzia mambo tofauti yanayoweza kukuvutia. Huwezi jua.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com