UNA KIPAJI CHA KUTANGAZA RADIO? MCHONGO HUU HAPA!

“Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu” siku zote najiulizaga “hivi wahenga walikuwa na busara kaisi gani? ” coz mpaka leo misemo kama huu, unaendelea kuishi na kudhihirisha kwamba jambo linaweza kufanikishwa kwa urahisi likifanyika kwa umoja. Hivi majuzi wakati nasikiliza kipindi cha radio cha Shujaaz kinachorushwa na kituo cha Abood radio nilihamasika kusikia mtangazaji DJTee akisisitiza vijana kuunda groups ili kusaidiana katika kitu anachokiita Nguvu moja.

Nguvu Moja ni kampeni ambayo inafanywa na Shujaaz kupitia kijarida chao kinachotolewa kila mwezi kikiwa na maudhui ya kuelimisha vijana juu ya fursa zinazowazunguka, na moja kati ya mbinu wanazotumia Shujaaz ni kuhamasisha umoja au urafiki wenye manufaa. Nimepata nafasi ya kufanya mahojiano na DJTee na kumuuliza kuhusu kampeni hii kupitia ukurasa wake wa Facebook, baada ya kukataa kuonana face to face.

vijana wenzangu wengi wameitikia wito wangu wa kufanya kazi pamoja, na mpaka sasa bado nafanya maandalizi ya kuipeleka hii kampeni kwenye level za juu zaidi, nimeona muitikio na nina imani itasaidia sana vijana kutengeneza biashara zao kwa umoja kitu ambacho kitanufaisha wengi” Alisema @DJTee255 alipozungumza na watupipo.com.

DJ huyo amesema kwamba idea aliipata tangu mwaka jana hivyo akaanza kuhamasisha vijana, “mwezi wa 12 nilibahatika kufanya kuhamasisha wenzangu kuunda makundi mengi… lakini manne kati ya hayo nimefanya nayo mahojiano kwenye kipindi na tukapanga mambo mengi. Moja kati ya makundi hayo wanajiita Full dose crew waliandaa tamasha la vipaji mkoa Kilimanjaro, na niliwapa sapoti ya kuwatangazia kwenye kipindi changu”. Ikiwa ni msukumo kutoka kwenye kampeni hii.

Kwa mujibu wa DjTee mwaka huu kuanzia mwezi April, vijana wenye vipaji na ndoto za kuwa watangazaji, watapata nafasi ya kushiriki kwenye shindano atakaloliendesha kupitia show yake inayosikika kila jumamosi kupitia vituo vitano vya radio… “Ninajua ni vigumu kupata nafasi ya kuonesha kipaji chako hasa kama unaishi vijijini sana, sasa nimeamua kutoa nusu ya show yangu kwa vijana kuonesha uwezo wao wa kutangaza kwenye presenter search”

Hii ni nafasi ya kipekee sana kwa vijana wenye ndoto za kuwa watangazaji wakubwa, unaweza kusikika na ukajikuta ndio unatoka kupitia shindano hili la kipaji cha kutangaza. Djtee amesema sharti kubwa kwa kijana ni lazima uwe kwenye group ili kupata nafasi ya kushiriki fursa hii adimu, hivyo ni vema ukajiandaa kwa kuunda group la watu wasiopungua watano au kujiunga na moja kati ya groups nyingi za Shujaaz ambazo zimeshaundwa Tanzania nzima ili uweze kushiriki.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com