10 PRESIDENTS WALIOONGOZA WAKIWA NA UMRI MDOGO

10. Theodore Roosevelt Jr

Alikuwa mwandishi, mtafiti, mwanajeshi na vitu vingine ambavyo hata sijui kiswahili yake kama naturalist… Roosevelt alikuwa Rais wa Marekani mwaka 1901 mpaka 1909. Huyu ndio alikuwa rais aliyewahi ku-run akiwa na umri mdogo zaidi. Kumbuka umri wa chini wa kuwa rais nchini humo ni miaka 35.

9. Joseph Kabila

Rais wa Congo ambaye alichukua madaraka baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila. Mnamo mwaka 2001 aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 29 tu.

8. General Gnassigbe Eyadema

Rais wa zamani wa Togo aliyeingia madarakani mwaka 1967 mpaka kufikia kifo chake mwaka 2005, just like normal rituals in Africa presidents (rule kama unchi ni ya kwako) Katika maisha yake ameparticipate kupindua serikali mwaka 1963 na wakati akiingia madarakani 1967. Jamaa kwa sababu alikuwa masta wa kupindua serikali haikuwa rahisi kumpindua na alishakwepa kifo kwenye ajali ya ndege, na jaribio la kumuua la 1993.

Huyu jamaa alikuwa anatembea na wanawake 1000 kwenye msafara ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu. Alikuwa anafanya sherehe ya kukumbuka siku aliyotaka kuuliwa kwa mara ya kwanza kila mwaka. Eyadema aliingia madarakani akiwa na miaka 29.

7. Rouque Gonzalez Garza

Aliiongoza Mexico kwa muda mfupi sana. Garza aliingia kwenye siasa akiwa ana miaka 22 na kushika urais akiwa na umri wa miaka 29. Jamaa baada ya kuongoza nchi kwa miaezi kama mitano hivi aliachia madaraka na kubaki kuwa mwananchi wa kawaida. Baadaye alifungwa na kiongozi mpinzani wake.

6. Yahya Jammeh 

Aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 29 tu… “mh inanifanya nione kwamba miaka hii ndio humfanya mtu atoke kimaisha” Jammeh aliingia madarakani kwa kupindua serikali mwaka 1994 na baadaye alichaguliwa kidemokrasia. Cha kushangaza jamaa mpaka mwaka 2016 alikuwa anataka kubaki madarakani baada ya kushindwa uchaguzi.

Vitu vya kukumbuka kutoka kwa rais huyu wa Zamani wa Gambia alikataza child marriages, alikuwa na imani kwamba anaweza kuponya HIV kwa kutumia mitishamba, na alitishia kukata kichwa cha yeyote atakayefanya ushoga.

5. Samuael Doe

Alishika madaraka kwa miaka 10 tangu 1980 hadi 1990. aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 28 tu baada ya kupindua serikali. Katika uongozi wake alikuwa rafiki mkubwa wa Marekani. Alifanikiwa kufungua milango kwa uwekezaji wa nje.

Ukiisha kwa upanga utakufa kwa upanga. Doe aliuawa kwa kuteswa na rais aliyempindua kwa kushirikiana na rafiki yake. Naskia kuna video inaonekana akikatwa sikio.

4. Kim Jong Un

Kiongozi wa nchi tukutu ya Korea kaskazini. Kim ameingia madarakani akiwa na umri wa miaka 28 tu na hivi karibuni ameshutumiwa kumuua kaka yake ambaye alikuwa kama tishio la pekee kwenye urais wake. Kim hajali dunia inataka au inafikiria nini maana kila wakimwambia asitengeneze mizinga ya nyuklia yeye ndio kwanza ana mimina chai na kupiga mluzi.

Huyu nimoja kati ya viongozi wachache wanaoijambisha Marekani kwa kuitisha na vita ya Nyuklia.

3. Michel Mikombiro

Akiwa na umri wa miaka 26 tu alifanikiwa kuwa rais wa Burundi. Jamaa alichukua madaraka kutoka kwa rafiki yake ambaye alikuwa mfalme. Mikombiro aliingia madarakani kibashite bashite mwaka 1966 baada ya mfalme kusafiri nje ya nchi na kumuachia nchi yeye ambaye alikuwa ni waziri mkuu tu. NOMA!

2. Valentine Stresser 

Alichukua urais siku tatu baada ya kusherehekea miaka 25 ya kuzaliwa kwake na kuwa rais mdogo zaidi aliyewahi kutokea enzi hizo. Alikuwa kwenye uongozi kwa miaka 4 tu kuanzia 1992 mpaka 1996 alipinduliwa na wanajeshi kwa kufanya kazi mbaya. Hivi sasa Stresser ni mtu wa kawaida na inasemekana ni masikini.

1. Jean Claude Duvalier 

Alishika uraisi akiwa na umri wa miaka 19 tu. HUUUH!!! Duvalier alikuwa rais wa Haiti baada ya baba yake kufariki mwaka 1971. Katika uongozi wake inasemekana aliuwa maelfu ya watu. Inasemekana alikuwa ni drug dealer na pia alikuwa anauza viungo vya watu. GRRRR

 

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com