CRAZY, UNBELIEVABLE THINGS DONE FOR LOVE – mapenzi uchizi

Kabla hujaendelea mbele hebu jiulize… Je umewahi kupenda katika maisha yako? Kama jibu ndio, je, umeshawahi kufanya kitu gani cha ajabu sana ambacho usingeweza kukifanya kama usingekuwa unampenda mtu? Mapenzi ni hisia zinazoweza kukufanya uchanganyikiwe.

Cheki vitu walivyofanya hawa jamaa kwa sababu tu ya mapenzi.

Kachoma msalaba kuzuia talaka

Jamaa mmoja kichaa wa mahaba kama walivyo vichaa wengine… uwezo wake wa kuhimili maumivu ya mapenzi ya mke wake uliisha, pale ambapo wife alikwishaleta karatasi za talaka kwa ajili ya jamaa kusign.

Fikra zake zikamtuma kumtisha mke wake kwa kuchoma msalaba mkubwa, nyuma ya nyumba yao, na kuacha ujumbe wenye maneno “ole wako umuache huyu jamaa”

Baadae polisi walichunguza na kubaini kwamba, mume ndio alichoma msalaba huo.

Kill her for me

Mwanamke anajulikana kama Lisa, aligundua kuwa mume wake anachepuka na baada ya kumchunguza, akamfahamu mwanamke ambaye aliyekuwa anachukua utamu wa mume wake. Kwa hasira Lisa akaamua kuchukua hatua kali ya kumuua… lakini hawezi kutumia mikono yake.

Alifanya uchunguzi wake na kukutana na Russel ambaye alikubali kufanya kazi hiyo kwa kiwango flani hivi cha pesa na Lisa akatoa dili. Baada ya Russel kukutana na dada ambaye alitakiwa amuue, alipigwa na butwaa kwa sababu huyu ni mwanamke ambaye alikuwa anampenda kwa muda mrefu, so akaamua kumpaka Tomato suace, na kumuagiza alale kama vile marehemu huku panga likiwa limebanwa kwapani, as If bado linajivinjari kwenye kifua chake laini.

Picha ilipigwa na kufikishwa kwa Lissa ambaye alikubaliana na kumlipa Russel… Baada ya miaka kadhaa siku moja kwenye Mall flani, Lissa alipigwa na butwaa baada ya kumuona Russel akiwa ameshikana mikono na yule mwanamke ambaye alimuua… kwa hasira Lissa akaenda kumshitaki Russel kwa utapeli, kitendo kilicho muweka yeye pia kwenye matatizo mapya maana alifunguliwa kesi ya kujaribu kuua.

Plastic surgery ili wafanane

Gerry na Stephanie wamependana zaidi ya kawaida labda au pengine ni umangáa wao tu ndio umewafikisha walipofika… Wanandoa hawa walitumia kiasi cha dola laki mbili kujifanyia plastic surgery ili wafanane. Haikutosha kulala na kufanya kila kitu pamoja mpaka mfanane?

Anataka mke amuachie matiti

Njemba moja kwa jina la Simon Williams lilivunja rekodi baada ya ku’file custody ya maziwa ya mkewe ambaye wamepeana talaka. Simon kwa ukichaa wake wa mapenzi ambao ni wa kimataifa, alikwenda mahakamani na kufuangua ombi hilo.

Simon amesema “Matiti haya nimekuwa nayo kwenye shida na raha, na ningependa kubaki nayo maana ndio ninakopata confort yangu” poor crazy guy… ina maana muda wote mke alikuwa hatoi mchezo bali anatoa boobs kwa jamaa… au pengine mke anaondoka maana huyu ndugu yuko obsessed na maziwa zaidi ya kitu yenyewe… sasa wa kazi gani?

Kufeki ajali

Watu kila siku wanatafuta mbinu mpya na idea za ajabu za kuwasurpise wapenzi wao na pete za uchumba. Baadhi wanafanikiwa kuwa surprise kweli kweli lakini hawawezi kumzidi nunda Victor.  Jamaa jioni moja alikuwa amepanga na mchuchu wake wakutane kwenye hoteli fulani ambapo mpenzi wake alifika kabla yake akawa anamsubiri.

Muda kidogo akasikia siren na kwa haraka akatambua kwamba, kwenye parking lot kuna ajali mbaya sana imetokea na mpenzi wake ndio alikuwa amekufa. Mbio mbio mpaka kwenye eneo la tukio na kuona mwili wa mtu wake umelala hapo chini ukiwa umetapakaa damu.

Aliporuhusiwa kuufikia na kuushika mwili wa Victor kwa uchungu… Ndipo jamaa akachomoa pete… Ofcoz alisema yes.

Shoot me to make her comeback

Kama unadhani wewe umeshafanya vitu vya ajabu kwa ajili tu ya dem aliyekuacha, basi kutana na mwenzako Jordan Cardela (20) Huku akiwa kwenye mapenzi mazito na baadaye kupigwa kibuti na msichana anayempenda… Jordan alishindwa kabisa kuvumilia maumivu ya mapenzi na ukizingatia umri wake, sio ajabu kitendo alichofanya.

Jordan aliandaa mpango wake na kumuomba rafiki yake mkubwa Michael ampige risasi mara tatu ili, girlfriend wake aliyemuacha akisikia amuonee huruma na kumrudia. Kwa Michael ambaye anaweza akashinda tuzo ya rafiki ndezi zaidi duniani, akakubali. Waka andaa eneo la kufanyia huo upuuzi wao.

Michael took the gun, aim at his friend’s arm and squeezed, Mlango wa chuma ukiufungua hauna huruma Jordan akapelekwa chini na kuanza kuvuja damu. Michael hakuweza kuendelea, japo Jordan alikuwa anahitaji kupigwa risasi nyingine. All in all Jordan akiwa Hospitali hakutembelewa na girfriend wake hasa baada ya kusikia kituko kilichotokea lakini polisi walikuwa nae sambasamba huku Michael naye akisaidia polisi. Japokuwa Jordan aliomba mwenyewe kupigwa risasi 3, sheria zinajua hicho ni kitendo cha uhalifu.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com