PEPE MADOCHI NA KABINTI KAGUMU – #ShujaazStory

Ukiwa mtoto sio mara zote unapata nafasi ya kumuimpress kwa uwezo wako wa kucheza vema zaidi ya wengine… Dogo Pepe kwenye jarida la Shujaaz stori yake ya kwanza mimi kuikamata ilikuwa hii aliyokuwa anawafyambiza wenzake chenga kama hana akili nzuri. Bila kujua kwamba kuna mtazamaji, sasa alipojua… ikawa shida zaidi. Sifa siku zote zinakuwaga na kikomo. Hasa kama unataka kuzitumia kuwa aibisha wenzako ili ujichukulie demu au kujikombea tu ujiko.Pale umejipiga kununua zawadi halafu uliyempelekea anakosa matumizi nayo. Hii inaleta zaidi lile somo la kwamba utafiti sio lazima uufanye unapotaka kuanzisha biashara pekee… bali hata wakati unapotaka kumpatia msichana zawadi lazima ujue ni vitu gani humfurahisha.
Somo moja ┬átu la kuchukua mpaka hapa ni kwamba… unapoamua kufanya kitu fulani lazima uwe na ujasiri wa kushindwa. Sio ujasiri wa kulifanya tu, maana asilimia kubwa ya vitu vyenye kuleta mafanikio au mageuzi huambatana na kushindwa na rejection zaidi ya mara moja. Ukiweza kuhimili kushindwa utaweza kujaribu tena na tena mpaka utakapofanikiwa.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com