JIFANYISHE MAMBO HAYA UONE MAISHA YAKO YAKIBADILIKA

Kwa mara ya kwanza kama umeawahi kusikia kitu kinaitwa “Law of attraction” Siwezi kutafsiri moja kwa moja lakini kwa kifupi ni kwamba hii ni aina ya maisha ambayo mtu anajitengenezea ili kuweza kuvutia aina ya matukio, ambayo kusababisha mabadailiko katika maisha yake.

Sheria ya mvuto unaweza kuiita kiswahili inatumika mara nyingi kwa watu wanaoijulia ili kuweza kuvutia vitu kama maisha mazuri na yenye furaha nk. Mara nyingi pia imekuwa ikizungumzwa na washauri kwamba ni sheria ambayo kila mtu anapaswa kuijua kwa vile hukaribisha furaha kwenye maisha yako.

Leo nimekukusanyia hizi Tips 4 ambazo ambazo ukizifuata utakuwa umejisogeza karibu na sheria hii ya mvuto na unaweza kusababisha mafanikio ya ndoto yako haraka kama upepo. Cheki…

Anza siku na mawazo chanya.

Ukisikia mawazo chanya au positive ni kwamba ufikirie mema zaidi ya maovu, uwaze utamu badala ya uchungu, uone mafanikio badala ya failure, ucheke badala ya kulia, utabasamu badala ya kununa, usikie raha badala ya karaha, uamini kushinda badala ya kushinda, upambane badala ya kukata tamaa na vitu kama hivi.

Wakati unaaamka asubuhi, akili yako inahama kutoka kwenye upande unaojulikana kama “unconscious abstract” ulimwengu usingizi na ndoto na kuingia kwenye hali ambayo ni ya kuamka, kile ambacho utawasha nacho gari kichwani kina maana kubwa sana kwa mafanikio ya siku yako.

Ndio maana wanasema siku njema huonekana asubuhi ukiamka kwa kufurahia na kuamini itakuwa siku nzuri na kweli unaiweka sehemu nzuri ya kuwa siku nzuri. Kuanza siku kwa positivity ni moja kati ya zawadi kubwa sana unazotakiwa kujipatia kila siku.

Jipatie kitu unachokipenda asubuhi, muziki, soma kitu nk.

Jitafutie wakati wa sasa

Present time maana yake ni wakati wa sasa, hivi sasa unaposoma hii… ni kitu gani kinatokea now? unahema? haraka au taratibu? je unaweza kuacha kila kitu uka-focus kusikiliza mapigo ya moyo wako? Yahesabu… Feel ile vibe ya wewe kuwepo, ondoa mawazo yoyote kichwani usimuwaze mtu yeyote waza NOW!

Hali ya kuwa “fully present” inasababisha uundwaji wa yale unayoyaaka kwa urahisi na haraka, kwa maana unakuwa kwenye state huru na ya furaha. Furaha ina nguvu kubwa katika uumbaji wa yale unayoyataka kwenye maisha. Furaha ni kama vile kusafisha roho na kubaki na afya nzuri ya moyo. Unahitaji hii.

Ni vizuri kufanya hivi mara kwa mara, japo sio rahisi sana. Anza kwa kuchukua dakika mbili tu kwenye siku yako bize… Acha kila kitu na ukae  ondoa kila unachowaza kichwani. Fanya kazi moja tu ya kuhema. Fanya hivi mara nyingi uwezavyo kwa siku moja ili uongeze muda.

Linganisha mambo

Mawazo chanya au furaha, huwa na nguvu kushinda karaha. Kila unapoenda, kuna force ambazo  ni negative unakutana nazo. Ili uweze kuwa na siku nzuri na kuachieve vitu vizuri unatakiwa kubadailisha au kupunguza hizo negativity kwa kutupia mawazo chanya, yenye furaha.

Jiulize swali kubwa kabla ya kulala

Kila siku kabla ya kulala jiulize “ni kitu gani kizuri zaidi kilichonitokea leo” Hapo tu unakuwa umeipa akili yako kazi ya kusakanya na kulinganisha yale mazuri yote na yaliyokufurahisha ili kupata zuri zaidi. hapa unajikuta akili yako inakuletea hata vitu vizuri ambavyo ulivisahau… hii ni hatua nzuri sana na uifanye kila siku kabla ya kulala.

Ongeza maswali haya

Vipi kama nikipata kiasi cha pesa ninachokitaka bial kutarajia?

Vipi kama kama yule dem/boy anayenivutia pale anafikiria the same kuhusu mimi?

Vipi kama mambo yangu yako hivi ili yaweze kubadilika na kuwa ninavyotamani?

Vipi kama ni nikifanikiwa goals zangu zote?

Mwisho kabisa anza kufanya majaribio na mwili wako. Kesho asubuhi ukifika eneo lako la kazi lazimisha tabasamu… tabasamu kwa kila unayekutana nae hata kama ndio unamuona kwa mara ya kwanza… onyesha sura ya furaha. Ukiona wengi kati ya hao wanatabasamu pia ujue una nguvu ya kubadilisha dunia.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com