BABA VANGA: MWANAMKE ALIYETABIRI, TRUMP, ISIS, OBAMA yuko on point

Mara kadhaa umesikia watu wakijiita watabiri na kutabiri mambo mbalimbali ambayo hayakutokea kama walivyobashiri. Now naomba nikupe stori ya mwanamama kipofu ambaye alifariki miaka zaidi ya 20 iliyopita, na ambaye alitabiri vitu vikubwa kama Urais wa Obama, kutokea kwa vita ya ISIS, Tsunami ya mwaka 2004 na mengine kama vile tukio la ugaidi lijulikanalo kama September 11.

Watu waliokuwa wakimuamini na kumfuata walimwita Nostradamus of the Balkans, lakini jina lake halisi ni Baba Vanga. Mwanamama huyu anaweza kuwa mmoja kati ya watu ambao wameishi na kuwa na uwezo wa kuona mambo ambayo yatatokea na yalikuja kutokea kweli na pengine yatakayotokea.

Yafatayo ni baadhi tu ya mambo ambayo pengine unaweza kuyafahamu ambayo Baba Vanga aliyatabiri na yakatokea.

Vita ya Syria na Waislamu Ulaya

Baba Vanga alitabiri kuvamia kwa waislamu katika bara la Ulaya, na akasema kwamba vita ya waislamu wenye imani kali, itakwenda kwa miaka mingi na itakuwa ni vita kubwa barani Ulaya kiasi cha kuliharibu kabisa bara hilo. Lakini pia alitabiri kwamba kutatokea vita ya waislamu wenye siasa kali nchini Syria.  Hivi sasa ISIS wamesababisha rabsha kubwa Syria.

Kutokea kwa Tsunami na Global warming

Utabiri huu ulifanyika mwaka 1960, na mama huyo alisema “Maeneo ya baridi yatabadilika na kuwa joto, kutatokea volcano na wimbi kubwa la maji litafunika miji na watu watapoteza maisha kwa wingi, Kila kitu kitapotea chini ya maji na kila kitu kitayeyuka kama barafu

Huu ni utabiri uliofanyika zamani sana, na ukiacha mbali Tsunami ya mwaka 2004, Sayansi pia inaonesha kwamba utakuja wakati ambapo maji yatavamia miji kutokana na Global warming.

Kuzama kwa manowari ya Urusi

Mwaka 1980 Baba Vanga alitabiri kwa kusema “Mnamo mwaka 1999 au 2000 meli ya urusi itafunikwa na maji na dunia nzima itakuwa juu yake”

Kweli watu wote waliokuwa kwenye manowari hiyo walikufa ingawa kulikuwa na juhudi za vikosi vya kimataifa vikijaribu kuokoa maisha ya watu hao.

Barack Obama kuwa rais

Baba Vanga pia mnamo miaka ya 1960, alitabiri kwamba rais wa 44 wa Marekani atakuwa mtu mweusi, na pia atakuwa ndio rais wa mwisho wa Marekani. Japokuwa utabiri huu wa kuwa atakuwa rais wa mwisho bado haujatimia, na Trump ndio incharge manyota, pengine labda kuna maana nyingine tofauti nyuma ya maneno haya.

Ulaya itaacha kuwepo

Baba Vanga pia alitabiri kwamba, ifikapo mwaka 2016 Ulaya itakoma kuendelea kuwepo, na hakutakuwa na maisha. Itakuwa ni kama sehemu yenye watu wasio na maisha. Ingawa mpaka hivi sasa utabiri huu bado haujatokea kama ulivyotajwa, lakini mwaka huo wa 2016 tulianza kuona mgawanyiko wa nchi za Ulaya, huku nyingine zikitoka katika Umoja wa Ulaya. Je hizo ni dalili za prophesy?

China kuwa Super power.

Zamani sana, mwanamama huyu alitabiri kwamba ifikapo mwaka 2018 China itakuwa the world superpower. Alisema wakati huu utafikisha mwisho wa mataifa nyonyaji duniani, na kwamba wanyonyaji watageuka kuwa third world.

Utabiri wa China kuwa superpower ulianza kuonekana baada ya IMF mwaka 2011, kutabiri kwamba ifikapo mwaka 2016 uchumi wa China utaupita ule wa Marekani, ambao ndio uchumi mkubwa zaidi duniani.

Je mwaka 2018 China kweli itakuwa world superpower? tusubiri.

Pamoja na tabiri nyingine nyingi ambazo zimewahi kutimia hizi zinazofuata ni zile ambazo bado wakati wake haujafikia na ni za kuangalia kwa jicho kali.

Mwisho wa njaa: Mwaka 2025 na 2028 njaa itakuwa imekomeshwa kabisa ulimwenguni na itakuwa ni historia forever. “Nadhani hii ni baada ya Tanzania na Kenya kujua jinsi ya kutumia vizuri ardhi kuzalisha chakula cha kutosha pia… right” LOL 

Safari za Venus: Akatabiri kwamba bianadamu watasafiri mpaka sayari ya Venus, kutafuta energy. Na kusema pengine wanaweza kuweka makazi huko.

Rome kuwa Capital of the Islam: Akatabiri kwamba ikifika mwaka 2043, waislamu watakuwa wamemaliza kuivamia Ulaya na mji wao mkuu utakuwa Roma.

Kuundwa kwa viungo vya mwili: Ifikapo mwaka 2046 binadamu atakuwa amesha-masta uundwaji wa viungo bandia vya mwili. Na hii itakuwa ndio tiba kuu.

Marekani kuivamia Ulaya: Ifikapo mwaka 2066, Marekani itavamia Ulaya na kujaribu kuwafukuza waislamu ambao watakuwa wameitawala, ili kurudisha ukristo.

Maisha ya chini ya maji: Mwaka 2130, mwanadamu atakuwa ameshajua jinsi ya kuishi chini ya maji, na hii itakuwa kwa msaada wa Aliens.

Kurudi kwa communism: Ikifika mwaka 2070, communism itarudi Ulaya na dunia nzima.

Mwisho wa dunia: Mwaka 3797, huu ni mwaka ambao Baba Vanga alitabiri kwamba dunia itafikia ukomo wake. Lakini akasema kwamba wakati huo binadamu atakuwa ameshajiendeleza kiasi cha kuhamia sayari nyingine na kuishi huko.

Dalili za kuisha kwa dunia zinaonekana wazi kutokana na vielelezo vingi vya kisayansi… Ntakuwekea makala hiyo tofauti siku nyingine. Lakini pia dalili za binadamu kuhamia katika sayari nyingine zinaonekana wazi kwa wanasayansi kama Mtoto wa Africa kusini ambaye kwa sasa pia ni raia wa Marekani Elon Musk, Ambaye kupitia kampuni yake ya Space X, anajaribu kuifikia Mars na ndoto yake ni kuifanya sayari hiyo kuwa kama dunia na wanadamu tuweze kwenda kuishi huko.

Endelea kukaa na watupipo.com coz kuna mengi sana yanakuja kwa ajili ya kukupa experience ya aina yake katika uandishi sanaa media na teknolojia.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com