NAFANYA BIASHARA YA KUSIMAMA KWENYE LINE (FOLENI) mil 2 kwa wiki

Kazi ya watupipo.com ni kukutanisha na stori za watu kama hii kutoka nchini Marekani. Robert Samuel ambaye kwa sasa ameanzisha kampuni inayofanya kazi za kusubiri kwenye line “foleni”kwa ajili ya watu wengine, na amini usiamini anatengeneza kiasi cha milioni 2 kwa wiki.

Baada ya kukosa ajira mwaka 2012, Robert alichangamkia tangazo la kumsaidia mtu kusimama kwenye line ili aweze kununua simu aina ya iphone. Basically mtu mwenye hela hataki kusubiri kwenye line lakini simu hizo ndio zilikuwa zinatoka na ziliuzwa kwenye duka la iphone pekee… so hata wenye hela walipanga foleni.

Baada ya kufanya mchongo wa kwanza Robert aliona fursa na kuanzisha kampuni inayoitwa  Same Ole Line Dudes, LLC – ambayo ni professional kwa kusimama kwenye foleni.

Jamaa ana wafanyakazi zaidi ya 12, ambao wengine ni part time na wameshasimama kusubiri concert tickets, pizza, iphone, na ishu zingine zote zinazohusu kusubiri kwenye foleni wao ndio wale wasee.

“nimeshawahi kupata dili la kusimama kwenye line kwenye shark tank, lakini kwa kuwa sikuweza kwenda nikampa mlemavu mmoja ambaye alifanya kazi nzuri” anasema Robert.

Ili kupata huduma unatakiwa kulipa advance ya $25 ambayo ni sawa na Tsh 25,000 au Ksh 1250… na baada ya hapo unatakiwa kulipa $10 kwa kila nusu saa ya kusubiri. Jamaa bado ana-make mkwanja wa kutosha na kwa sasa na haoni sababu ya ku-upgrade biashara yake na kutengeneza app yake.

So kama unaweza kuifanya hii kazi kwenye jamiii yako sio mbaya ukajaribu pengine kuna vijana wanasubiri kuajiriwa na wanalalamika hawana kazi, tell a friend to tell a friend.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com