Listen Live!

UTUNDU WA SELFIE DRONE CAMERA, INAYOUZWA KICHOYO NA APPLE.


Ndio kwanza kumekucha kwenye ulimwengu wa wauza sura, na hata wale ambao wanapenda tu kupiga picha za vitu wanavyofanya bila kungángána na Camera au kupidua pindua simu. Hover Cam Passport, ndio habari ya dunia hivi sasa.

Kwa kutumia Camera hii ambayo inapaa na kukufuata kila unapokwenda bila ya wewe kuiongoza unaweza kurekodi video na kila kinachoendelea katika ulimwengu wako na picha zote zikaji-save kwenye app malumu ya Hover Cam ambayo uta-install kwenye simu yako.

Kwa kutumia teknolojia ya AI (advanced facial recognition) Hover Cam itakuwa na wewe kwenye shida na raha, huku ikikupiga picha wakati uko bize na mambo yako… lakini pia ukabadilisha kwa kutumia simu yako either kurekodi video, ambayo inarekodi kwa kiwango cha 4K au still picture ambayo utaipata kwa 13MP chaguo ni lako.


Jinsi ya kuitumia ni cha mtoto tu, unaikunjua kama vile unatanua mabawa na ku-press power button then kitu kishapaa. Sasa selfie stick tupa kule, maana zile picha zote za 360 spin, Orbit, Body tracking sasa ni possible. Hii ni level nyingine ya drone kutoka kwa kampuni ya Zero Zero Robotics

Hivi sasa Camera hii ya kisasa zaidi imeingia sokoni na kama ujuavyo wachoyo wa Apple ndio wanaiuza kupitia Apple.com pekee kwa sasa bei yake ni $499.95  au Ksh 50,000 au Tsh 1,000,000 .

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com