REVIEW: WIMBO “SHOW ME” – HARMONIZE FT RICH MAVOKO – #bythepeople

Watupipo, muda mfupi tu kabla ya kufungua kurasa na kuandika hii, nilikuwa kwenye mtandao wa jamii forum nikakutana na “Uzi” mmoja kuhusu kushuka kwa muziki kwa Rich Mavoko. Mtu aliyeandika uzi huu akasema kwamba yeye ni mpenzi wa  muziki wa Rich, lakini, ameshuka ki-muziki kwa kuwa alihamia WCB, kurudi kwa Millard Ayo nikakutana na video ya wimbo mpya wa Harmonize na Rich Mavoko. Hatariiii.

Maoni yangu kwenye huu wimbo mpya unaoitwa “Show me” ni mkali sana. Moja kati ya hit ambazo zinaweza kufunika kama Muziki ya Darassa ft Ben Paul.  Lakini kwa wale wanaopingana na hii ngoja nikukutanishe na maini ya watu wengine waliosikiliza na kuangalia video  ya Show me – Harmonize ft Rich Mavoko. Labda unaweza kubadili mtazamo.

I do not speak swahili but, hii ngoma ni kali….!

Haka kamsemo ka I dont speak swahili lakini nimependa hii video, sasa kameshika kasi Youtube… watu wanafanya aliwahi kuanzisha mtu baada ya kuona watuwasiopenda kiswahili wakisema “I do not speak swahili but I love this song” Wabongo wakaweka version yao sasa ndio hii…
Ukiachana na demu wa Somalia ambaye ame-fall in love, baada ya kusikia ametajwa kwenye ngoma. Haka katabia kanafanyaga wasichana wapenda muziki kukunwa na mziki husika. Taja majina umewapata.

Video kali

Views 1000 times every half an hour, hii ni trend nzuri, rate ya Likes na Dislikes as of now ni 2004 kwa 107, people like his video more. Show me ni video ya kisasa na imekuja wakati muafaka ambapo matumizi ya video vixens ilikuwa binafsi imeanza kunikinaisha kuangalia video. Kila video anakuwa yule Lulu duh!

Video vixen

Mrembo maarufu Model na famous video vixen Amanda tofauti na zilivyo video nyingi zinashirikisha models wale wale kila siku.
Fans kutoka mtandao wa Youtube wamemzungumzia pia model huyu na kwenye ukurasa wake wa Instagram amepokea love kibao na mafisi pia kumkaribisha Tanzania.

 

Mti wenye matunda

Vera Sidika ametajwa kwenye hii ngoma japo hajaonekana. Kenyans on youtube wameonesha mapenzi yao kwa Model huyo na video vixen maarufu Africa. Hii inaniambia Watanzania pia inabidi kujivunia uwakilishi unaofanywa na wasanii isichukuliwe poa… shabiki akiwachukulia poa, hata serikali itafanya hivyo.

Siku zote kila kizuri kina makosa yake kuna waliosema hii beat iliyotumika hapa inafanana na beat aliyotumia Edy Kenzo wa Uganda. Inzawezekana kuna ukweli lakini producer Africa wamekuwa na hii tabia kwa kuwa wakati mwingine wanakua inspired kwa kazi za wenzao na sio kitu kibaya.

DjB wa Shujaaz na Mark register

Huu ni msemo unautumika sana na kijana mtangazaji wa kipindi cha Shujaaz radio show kinachorushwa Milele fm jumapili 8PM – 9PM. Fans pia wnatumia huu msemo kwenye comment za “show me”

Recommendations

Harmonize ft Rich Mavoko imekuwa good suprise kwangu mimi binafsi maana nilikuwa ana reflect na kujiuliza WBC wana jipya kweli? Hili sio jipya bali ni upgrade ya hali ya juu. Show me ft Rich Mavoko ni jiwe kali pasaka hii.

Watch Show me – Harmonize ft Rich Mavoko here

Acha comment yako pia, watupipo.com itapita tena kukusanya maoni yako. Je ni video kali na ngoma yenyewe vipi? Je Harmonize anasound kama Diamond Platnumz? I think so too. Anyways enjoy god music and support kwa kununua hii ngoma hapa WCB 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com