PICHA UNAZOPOST ONLINE Vs TABIA ZAKO

Selfie Mtu mwenye post nyingi za selfie inaonesha kuwa mtu huyu anapenda sana attention, anahitaji sana recognition and approval ya watu wengine. Huyu ni mtu ambaye kwa English unaweza kumuita self-cantered, na anajali sana muonekano wake. Sexy photos Ukiachana na wale wana mazoezi wanaoonesha misuli. Msichana ambaye amejaza picha za muonekano wa umbo lake, anaweza kuwa anatuma ujumbe kwa dunia kwamba; Ni mwanamke huru, yuko tayari kujaribu “mambo” (watu wazima wanaelewa). Msichana kama huyu mwili wake unatumika kama mtego au ulimbo. Kama unahitaji serious relationship pengine inabidi kumchunguza zaidi msichana anayefanya hivi, coz anaweza asiwe tayari ku’settle down. Couple photos Ukiwa na picha hizi nyingi kwenye account yako inabidi ujiulize; je unaziweka ili kuonesha kuwa… unapendwa, hauko peke yako? Wengine hufanya hivi kuweza kuwachapa fimbo wapenzi wa zamani ex’s au wale wenye wivu wajinyonge. Group photos Mtu akiwa na picha nyingi za yeye akiwa na marafiki, inaonesha kuwa mtu huyu ana thamini sana marafiki, lakini pia mtu huyu anaweza kuwa ni mtu mpweke “loney” na anahitaji kuonesha kwamba I belong to this group. Picha za utotoni Mtu ambaye kila mara anaweka picha zake za enzi akiwa mtoto. Huyu anaonesha kwamba amechoshwa na maisha ya utu uzima… Kukabili vitu kama mikopo, heart break na majukumu mengine sio kitu cha mchezo mchezo. Mtu huyu anaweza kuonesha kwamba anahitaji kuhudumiwa kama mtoto… Msichana wa namna hii uki’date nae lazima uwe kama dad yake. Umpakate, umbembeleze kulialia kwingi… so ujipange kabisa. Wild animals Kama mtu ni mpiga picha akiweka picha za aina yoyote ikiwemo za wild animals itaonesha kuwa ni kazi yake. Ikiwa mtu wa kawaida anaweka picha za wanyama wakali, kama Simba, Wolf kwenye wall na profile picture yake, basi anatamani kuonekana kuwa strong lakini kwenye maisha ya kawaida sio. Kwa mwanamke akiwa anaweka picha za paka na viwanyama vingine, ina maanisha kwamba mwenye account ana ka’utoto ndani yake, sio kwa nia mbaya though. Nature Hii inaonesha kwamba mtu huyu anapenda nature au pengine amechoshwa kabisa na maisha ya ulimwengu wa magari majumba na frustrations za jiji kwa ujumla. Kama una mtu kama huyu mpe nafasi yake apumue kidogo au mpeleke vacation la sivyo anaweza kukupasukia. Expensive stuff Mtu anayeweka picha zake akiwa na vitu vya kifahari inaweza kumaanisha vitu viwili. 1: Ni kuonesha kwamba unatamani kuwa na vitu kama hivyo (desire) 2: Kuonesha success zako kwa nia tofauti… either ili uonekane juu zaidi ya wengine au kuonesha kwamba hukutegemea kuwa ungefika ulipofika. Extreme Photos Mtu wa namna hii anaonesha umahiri, strength, masculine, au ujasiri wake. Picha za kazini Mtu anayeweka picha kama hizi huonesha kwamba kazi yake ni muhimu sana, na pengine ana mkakati wa kufika mbali.   Natural photosKuna watu unakuta hajabadilisha picha yake ya profile kwa muda mrefu. Mtu kama huyu anakuwa hana umuhimu wa kuonesha maisha yake kwenye social media kwa sababu ameridhika na maisha nje ya social media. Mara nyingi mtu kama huyu ndio hutumia social media kuwasiliana na marafiki zake na kufanya biashara. Huu ni utafiti usio rasmi na umeambatana na maoni binafsi. Je wewe uko kundi gani na maoni gani uko nayo juu ya rafiki zako?

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com