MAMBO 10 TOKA KWENYE RIPOTI MPYA YA ELIMU TZ

Ripoti imeachiwa rasmi mwezi April inaonesha tafiti iliyofanyika kwa kipindi cha mwaka 2011 – 2015.

1 :Uwezo wa kusoma kuhesabu na kuandika bado uko chini na haujafikia kiwango kinachotakiwa au kama ilivyotarajiwa.

2: Hakuna mabadiliko makubwa kwenye matokeo ya kujifunza kwa kipindi chote cha utafiti 2011 – 2015.

 3 : Viwango vya ufaulu na kujifunza kwa somo la Kiswahili vimeongezeka na kuendelea kuzidi somo la Kiingereza lakini pia disaster ipo kwenye somo la hesabu ambalo bado limesimamia pale pale kama mnara wa askari.

4 : Akina mama waliopiga kitabu kiasi wameendelea kuwasaidia watoto.

5 : Bado kuna tofauti kubwa kati ya wanafunzi wa mjini na vijijini. Wa mjini wameonekana kukaa kwenye nafasi nzuri.

6 : Japo kuna taarifa za watoto wengi zaidi kuandikishwa baada ya serikali ya awamu ya 5… ripoti inaonesha kuwa tatizo liko hadi kufikia mwaka 2015.

7 : Wanafunzi vijeba wameongezeka zaidi.

8 : Lazima tupongeze jitihada za kupatikana kwa vitabu. Kumeonekana mabadiliko makubwa tangu mwaka 2013 – 2015.

9 & 10 : Chakula na utoro… mwalimu na mwanafunzi wote watoro.

 

Ripoti hii imechapishwa na Uwezo ikionesha trend ya kujifunza kwa level ya primary school katika shule za serikali.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com