EAST AFRICA PRESIDENT’S SIKU YA WAFANYAKAZI – may 1st announcements

Leo ikiwa siku ya wafanyakazi duniani, mataifa mengi yamesherehekea kwa mapumziko huku viongozi mbalimbali wakitumia nafasi hii kuzungumza na wafanyakazi. Katika mataifa makuu ya Afrika mashariki viongozi wakuu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda wamekutana na wafanyakazi na haya ni mambo makubwa waliyozungumzia.

TANZANIA – JOHN MAGUFULI

Maadhimisho ya siku hii yalifanyika katika mji wa kitalii wa Moshi, mkoani Kilimanjaro na rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi. Katika hotuba yake Magufuli amechukua nafasi kuwakumbusha wafanyakazi azimio lake la kujenga Tanzania ya viwanda (uchumi wa viwanda) lakini pia kuelezea mambo anayyachukia kama rushwa na udanganyifu unaofanywa na wafanyakazi wa serikali

Magufuli ia ametangaza kwamba serikali yake baada ya kumaliza zoezi la kusafisha wafanyakazi hewa, itaendelea na zoezi la kupandisha wafanyakazi vyeo na pia kuongeza mishahara. Alisema kwamba zoezi hili ambalo hufanyika kila mwaka lilisimama ili kupisha usafishaji wa wafanyakazi hewa.

KENYA – UHURU KENYATA

Katika maadhimisho haya ya Mei mosi, Rais Kenyata aliyekuwa mgeni rasmi katika viwanja vya Uhuru Park, alitumia siku hii kutangaza ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 18. Katika hotuba yake HE Kenyata alisema serikali yake inaondoa kodi kwa wafanyakazi wanaolipwa kima cha chini cha shilingi 13,475.

My government is concerned with the large number of Kenyans looking for jobs and those struggling to provide for their families, thus my government has offered 18 per cent increase in minimum wage, Alisema rais Kenyata.

Hata hivyo kabla ya siku ya wafanyakazi, Federation of Kenya Employees ilimuomba rais asitangaze ongezeko la mshahara siku ya wafanyakazi, ili kupisha adjustments za nyongeza ya mwaka jana ambayo bado haijamaliza kufanyiwa marekebisho.

UGANDA – YOWERI MUSEVENI

Katika Hotuba yake ndefu rais Museveni yeye amewataka wafanyakazi wa serikali ya Uganda kuacha uzembe kazini. Alisema kwamba kuna wafanyakazi wanafika kazini late, na badala ya kufanya kazi wanaishia kuchati kwenye mitandao ya facebook na Whatsapp.

Pia rais Museveni amewaasa wananchi wa Uganda kuacha kunywa pombe kiasi cha kupindukia, kwa maana wanasababisha nguvu kazi kupotea. Jingine kubwa katika hotuba ya Rais Museveni ni rushwa. rais Museveni alisema kwamba wale wanaochukua rushwa wanawanyima vijana ajira na kwamba mamlaka hazitasubiri kupata ushahidi kamili kumwajibisha mla rushwa.

UKIWA NA CHOCHOTE CHA KUONGEZA KWENYE ARTICLE HII, PLEASE FEEL FREE KUONGEZA HAPO CHINI. watupipo.com

 

You may also like...