SAMUEL UMESHINDA KSH MIL 221 KUTOKA SPORTPESA

Nimestushwa na habari niliyosikia hii leo, kuhusu mshindi wa kiasi cha Ksh 221 za bahati na sibu kutoka kampuni ya uchezeshaji bahati na sibu ya Sportpesa. CEO wa kampuni ya sportpesa Ronald Karauri alikuwa mwenye furaha kumpigia simu Samuel ili kumpa habari hizo ngumu kuaminika kirahisi.

Ushindi huu wa Samuel, ulisababisha watumiaji wa mtandao wa Twitter, kushusha msururu wa tweets za kumpongeza, huku wengine wakiomba awagawie angalau kiasi kidogo waweze kurekebisha maisha yao.

Samuel ameshinda kiasi hicho kikubwa zaidi cha bahati na sibu Afrika, baada ya kutabiri jumla ya michezo 17 kwa usahihi, na kwa hilo tu anakuwa ndio winner mkubwa zaidi aliyewahi kutokea Africa.

Kiasi hicho ni sawa na Tanzania shilingi Bilion 4 au Dola milioni 2. Hii inamaanisha Samuel ameshakuwa milionea kidunia kutokana na mchezo ambao baadhi ya watu wanauona kama ni wizi au uvivu wa kujituma kwa wanao uendekeza.

Hii itakuwa ni morali mpya kabisa kwa wachezaji wa bahati na sibu kwa kuwa inajenga imani na hamasa ya utajiri hasa kwa vijana, japokuwa bahati kama hii iliyomuangukia Samuel sio rahisi kutokea katika maisha ya mcheza kamari wa kawaida.

Wakati kukiwa na maelfu ya watu wanalalamika kupoteza mitaji, wengine savings zao za maisha kama ilivyokuwa kwa kijana Kanjunju John kutoka Tanzania, ambaye alionekana akilia kwenye mitandao baada ya kupoteza mtaji wake kutokana na betting, wengine ndio kwanza wanaongeza spidi katika kuweka pesa zao na bett ili watoke kimaisha.

Leo itakuwa ni siku ya pekee sio tu kwa Samuel, bali ni siku kubwa pia kwa kampuni ya Sportpesa ambayo imeanzishwa mwaka 2014 na kuonesha nia ya dhati ya kuchangia kwenye ujenzi wa soka nchini Kenya. Kampuni hiyo mwaka 2016 ilifunga deal na kampuni ya Southampton ili kusaidia kunyanyua vipaji vya wanasoka wachanga, na pia kuweka nia ya kusaidia timu ya Taifa ya Kenya kucheza kombe la dunia mwaka 2022.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com