GNAKO : HIKI NDIO KILEVI CHANGU NA SIDE HUSTLE YANGU

Msanii Gnako ambaye anaweza kuitwa mkali wa Chorus nchini Tanzania mpaka hivi sasa, ametuambia mishe anayoipiga nje ya muziki kuwa ni utengenezaji wa Kahawa. Akifanya mazungumzo kwenye kipindi cha vijana cha Shujaaz radio show kinachoendeshwa na DJ maarufu DJTee, akishirikiana na H2K na Ikky, Gnako ameelezea utofauti wa kahawa wanayoitengeneza na Kahawa nyingine zilizoko sokoni.

“Kahawa yetu ya Nuru Caffee, ni tofauti sana na nyingine maana inarahisisha matumizi, imechanganywa tayari na maziwa, na sukari hivyo mnunuzi anatakiwa kuchemsha maji tu na kuenjoy” alisema Gnako ambaye kwa sasa anatamba na ngoma mbili kali ambazo ni “ya kulevya” akiwa na Joh Makini na Nikki wa pili, pamoja na Go Low akiwa na Jux.

Gnako pia alimwambia H2K kwamba yeye ameamua kujiingiza kwenye biashara ya kahawa kwa sababu ni kinywaji anachokipenda sana, na kwa vile yeye hatumii kilevi aina yoyote, amekuwa akifurahia kahawa akiwa studio, na katika mishe zake nyingine.

“Tunatarajia ndani ya miaka mitano, Nuru Coffee itakuwa kubwa na pengine tutakuwa na kiwanda cha Kahawa” – Gnako.

Habari hii iwafikie vijana wanaoingia katika muziki hivi sasa kwa maana mbili, 1) Unapopata nafasi ya kuvuma, ni muhimu ukawekeza jina lako na pesa zako kwenye biashara ambayo haitegemei muziki. Hii itakusaidia kuendelea kupiga hela hata pale biashara ya muziki ikishuka. Kitega uchumi kitakusaidia pia kuendelea kuishi kama hadhi yako ilivyo.

Kingine cha msingi ni kwamba sio lazima utumie kilevi ili kufanya vizuri kwenye muziki, hii inadhihirishwa na Gnako ambaye mara zote amekuwa mkali wa melodies huku akiwa anatumia Kahawa pekee. Ukiingia ndani kabisa ya Music Industry duniani, utashtushwa na idadi ya wasanii wakubwa ambao hawawezi kufanya muziki mzuki kabla ya kutumia pombe, na vilevi vingine.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com