AJALI NYINGINE TZ, WETANGULA HAGOMBEI KENYA? na stori zingine


Msiba mkubwa uliotokea Tanzania siku ya Ijumaa na kuchukua maisha ya watu 32 umeifanya Afrika Mashariki kuzama kwenye Weekend yenye Simanzi. Leo jumatatu May 8, Watanzania wakiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha na makamo wa rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwapa pole wazazi na ndugu waliopoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo mbaya.

Basi dogo lililokua limebeba wanafunzi wa darasa la saba lilipoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye korongo na kuua wanafunzi hao 29 pamoja na dereva na walimu wawili.

Kiongozi wa chama cha upinzani Moses Wetangula ametajwa kutoshiriki kutetea kiti chake katika uchaguzi ujao Agosti 8, Wetangula ametajwa kupoteza nafasi hiyo kwenye chama chake baada ya kiongozi msaidizi wa chama hicho Boni Khalwale kusema kuwa Wetangula hatatetea kiti chake.

Wetangula amekuwa katika harakati za kuingiza muungano wa vyama vya upinzani NASA madarakani huku akiahidiwa kupata cheo cha deputy premier incharge of economics endapo chama hicho kitaingia madarakani.

Pengine ni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea katika maeneo mengi nchini Tanzania, lakini mambo sio shwari baada ya ajali kadhaa kuzikumba jamii za mikoa mbalimbali na kupoteza maisha ya watu wengi. Mjini Tanga kumetokea ajali nyingine ikilihusisha basi aina ya Coaster lililokuwa likisafiri kutoka Tanga mjini kuelekea wilaya ya muheza kuligonga Loria lililokuwa limepaki na kuchukua maisha ya watu wanne.

Wakati huo huo mkoani Morogoro ajali nyingine imejeruhi watu 10. Huku waandishi wa habari wakiombwa kufanya uchunguzi na kufichua vyanzo vya ajali hizi.

Baada ya mwezi huu kutoa Ksh mil 221 kampuni ya Sportpesa imefungua rasmi tawi jipya Tanzania. Hii ni habari nzuri kwa watandikaji mikeka. Rummors kutoka mitaa ya Nairobi ni kwamba Sportpesa inatarajia kuidhamini klabu ya watoto wa Jangwani Yanga.

Wakati wanaharakati mbalimbali na mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike yakifanya kazi ya kupiga vita ndoa za watoto… Waziri mwenye dhamana ya jinsia na na watoto Dr. Hamis Kigwangwala amesema kwa sasa ni vigumu kupiga marufuku kabisa ndoa hizo nchini Tanzania. Amesema hatua hizo zinatakiwa kufanywa kwa awamu ili kufanikisha uharamishwaji wa ndoa hizo.

hata hivyo Kigwangala amesema sio rahisi kuzipiaga marufuku kabisa ndoa hizo, na kutaka kuwekwa kwa mfumo utakaozikubali baadhi ya ndoa za utotoni kutokana na mila za makabila mbali mbali.

Baada ya kuangushwa kwenye hatua za kwanza kabisa za kuwania tena kiti cha ubunge, kaka wa mwanasiasa na mgombea urais wa muungano wa NASA Raila Odinga ajulikanae kama Oburu Odinga amesema sasa yuko tayari kumsapoti kaka yake katika kinyangányiro cha urais kitakachofanyika Agosti 8.

Benki kuu ta Tanzania BOT imefuta leseni ya benki ya FBME. Benki hiyo imekutwa na hatia ya kutakatisha fedha nchini marekani na mtandao wa FinCEN. Mwka 2014 benki hiyo ya kimataifa ilikutwa na hatia na hivi karibuni mahakama jijini Washngton imefikia hukumu na kutokana na kwamba benki hii ni ya kimataifa, haitaruhusiwa kufanya kazi nchini Tanzania.

Pamoja na machafuko yaliyotokea nchini Afrika kusini, Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma anatembelea Tanzania. Zuma aliyekaribishwa na mwenyeji wake rais Magufuli wanatarajia kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa biashara.

Kampuni kubwa zaidi ya Nakumat bado inakabiliwa na ukata kutokana na upungufu wa mauzo. Mwanzoni mwa mwaka Nakumat ilifunga baadhi ya store zake kadhaa na sasa imetangaza kuendelea kufunga baadhia ya maduka yake.

May 8, uongozi wa kampuni hiyo ulitangaza kwamba mchakato unafanyika kufunga baadhi ya maduka yasiyokuwa na mauzo mazuri ili kuwezesha ufunguzi wa maduka katika maeneo ambayo biashara ni nzuri.

Endelea kutembelea watupipo.com kwa ajili ya mkusanyiko na summary ya habari zilizoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali Kenya na Tanzania.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com