TOP 10 : NCHI ZINAZOZALISHA MAHINDI ZAIDI DUNIANI

Wakati Africa mashariki inajaribu kukabiliana na matatizo mengine kibao (hasa ya mivutano ya kisiasa) ardi yenye rutuba bado haijaweza kuajiri asilimia kubwa ya vijana. Kwa kuwa ugali ni chakula muhimu sana hasa kwa nchi za Kenya na Tanzania, nimekukusanyia idadi hii ya nchi 10, zinazoongoza kuzalisha mahindi tofauti kabisa na ambavyo ungetarajia.

10: AFRIKA KUSINI

Nchi pekee barani Afrika kwenye listi hii. Mwaka 2014 – 2015 SA ilizalisha kiasi cha 15.5 metric tons na kuipa nchi hii nafasi ya kumi ya uzalishaji wa mahindi duniani. Kiasi kikubwa cha zao hili kinazalishwa maeneno ya kaskazini-Mashariki mwa nchi, Guateng, na Kasazini-Magharibi. Mahindi hulimwa kwa wingi msimu wa September na December na harvest hufanyika kuanzia mwezi April.

9: FRANCE

Kwa mwaka nchi hii inazalisha kiasi cha 17 metric tons na karibu maeneo yote nchini Ufaransa yanalima mahindi. Lakini pia kiasi kikubwa cha mahindi kinatoka maeneo ya kusini. Mahindi kupandwa mwezi April – May na kuvunwa mwezi September – November. Pamoja na kuzalisha kwa wingi zao hili wafaransa hawatumii sana mahindi hivyo kiasi kikubwa huwa exported, na hii inaifanya nchi ya Ufaransa kuwa namba tatu kwa kusafirisha mahindi duniani.

8: INDONESIA

Pamoja na kuwa nchi hii ilizalisha kiasi cha 18.5 metric tons mwaka 2013 ilitumia kiasi cha 20.7 metric tons the same year na kusababisha kiasi kingine kuingizwa toka nchi nyingine. Indonesia kwa sasa inazalisha kiasi cha 19 metric tons na inatumika zaidi kulisha mifugo ambayo ni sector inayokua kwa kasi nchini humo. Kwa sasa ikomipango ya kukuza uzalishaji wa mahindi na hiiitachangia uharibifu wa natural forests an wanyama mwitu. Hawa jamaa hawapendi ujinga.

7: MEXICO

Mexico bado inahitaji kuagiza mahindi nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya kulisha mifugo ambayo ni sector inayokua zaidi nchini humo. Mwaka 2013 ilizalisha kiasi cha 22 metric tons na mwaka 2014 ilizalisha kiasi cha 32.6 metric tons na bado kiasi hiki hakitoshi kutumika kwa binadamu na wanyama. Kiasi kikubwa cha mashamba nchini humo (61%) kinatumika kuzalisha mahindi na kuna seasson mbili za kilimo hiki. Mexico bado inahitaji kuongeza uzalishaji wa mahindi ili kukidhi hitaji la kulisha wanyama nchini humo.

6: UKRAINE

16% ya export ya mahindi duniani inatokea nchini Ukraine, ndio maana nchi kama Iran, S. Korea, Japan China na nyingine zinategemea mahindi kutoka kwa nchi hiyo. Pamoja na kuwa ni nchi ndogo, Ukraine inazalisha 39.2 metric tons za mahidi kwa mwaka na kutumia kiasi kidogo tu ndani ya nchi. Kitu cha msingi kinachochangia uzalishaji huu ni ardhi yenye rutuba sana wa chenzem au udongo mweusi.

5: ARGENTINA

Kiasi cha uzalishaji mahindi nchini humo kinafikia 40 metric tons kwa mwaka. Inakadiriwa kaisi cha hekari milioni 5.88 zimelimwa zao la Mahindi. Serikali ya nchi hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kusaidia wakulima kuzalisha kwa wingi zao hili.

4: INDIA

Kiasi cha 42 metric tons za mahindi kinazalishwa nchini India kwa mwaka. Msimu wa mvua May na July ndio wakati ambao wakulima hupanda mahindi na kuvunwa kuanzia mwezi November hadi July. Eneo la kaskazini mwa nchi hasa maeneo ya Uttar Pradesh, Bihar, Himachal Pradesh, Rajasthan ndio huzalisha kwa wingi zaidi mahindi, lakini pia Uttar Pradesh ndio eneo linalozalisha mahindi kwa wingi zaidi, kiasi cha 16%.

3: BRAZIL

Msimu wa kupanda mara nyingi huanzia mwezi January mpaka March, na style ya nchi ya Brazil hulima mahindi kwa kupanda maharagwe ya soya pembeni ili kusaidia kuongeza nitrogen kwenye udongo na kuzalisha mazao mazuri zaidi. Brazil ni nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa zao hili na kiasi cha export kimongezeka kutoka 1.10 metric tons mwaka 2015 mpka 5.37 mwaka 2016 na kuongez foreign currency toka $206.4 million in February of 2015 hadi $892.2 million in February of 2016.

2: CHINA

Kwa miaka michache iliyopita nchi hii imeongeza uzalishaji wa mahindi kwa kiasi cha 125%. Hivi sasa china inazalisha 224.9 metric tons kwa mwaka kiasi ambacho kimefanya mahindi kuwa zao linalozalishwa kwa wingi zaidi nchini humo likifuatiwa na mchele. Kiasi kikubwa cha zao hili kinatumika kulisha mifugo. Kiasi kikubwa cha wachina wanahamia mijini na ongezeko kubwa la hitaji la nyama duniani limechangia china kuongeza uzalishaji wa mahindi kwa ajili ya mifugo. Mwaka 1940 asili robo tatu ya mahindi yalitumika kwa ajili ya chakula cha binadamu lakini hivi sasa 60% ya mazao ni kwa ajili ya mifugo na 10% ndio hutumika kwa direct human use, wakati 30% inatumika kuzalisha bidhaa viwandani kama pombe nk.

1: USA

Miaka nenda miaka rudi, nchi hii imeongoza kwa kuzalisha mahindi duniani, ambapo kwa mwaka huzalisha kiasi cha 377.5 metric tons. 205 ya mavuno yanatumika nje ya marekani. Zao la Mahindi lilianza kulimwa maelfu ya miaka iliyopita wakati huo likijulikana kama teosinte mpakani mwa Marekani na Mexico. Hivi sasa Iowa inaongoza kuzalisha mahindi kwa wingi zaidi ikifuatiwa na Ilinois na Nebraska. Marekani inatumia kiasi cha hekari milioni 92 kwa ajili ya kilimo cha mahindi pekee.

Japo nchi nyingi kwenye hii listi hazitumii mahindi kutengeneza ugali kama sisi huku Afrika mashariki lakini zimeweza kukuza na kupata mazao mengi zaidi kwa ajili ya kulisha mifugo ili kupata mifugo bora zaidi. Kenya na Tanzania pamoja na kutegemea sima kama chakula muhimu sana kwa familia, imekuwa ni vigumu sana kuzalisha kiasi cha mahindi yanayoweza kulisha familia zetu kwa mwaka mzima bila kulia lnatia uchungu sana ukipita katika miji mbalimbali East Africa, unakuta vishamba vidogo vidogo vya mahindi ambavyo wakulima wamejitahidi kubahatisha, huku wakifunga na kuomba ili mvua zimalize msimu vizuri na kuwapa mavuno angalau ya kutosha familia zao ingawa mara nyingi hujikuta wakilia kutokana na hali ya heza kubadilika.

Tatizo kubwa la nchi hizi za Afrika mashariki sio ardhi maana ardhi iko ya kutosha, tatizo kubwa ni elimu kwa wakulima pamoja na nyenzo zinazokwenda na wakati zinazoweza kuwasaidia wakulima kuzalisha kibiashara zaidi ya kufikiria kuzalisha kwa ajili ya familia. Pengine ni wakati muafaka kwa Jumuia ya Afrika mashariki kuunda mfumo unaoweza kusaidia wakulima katika ukanda huu kuzalisha kwa ajili ya wananchi zaidi ya 150 milioni katika jumuia, ambao chakula chao kikubwa ni ugali.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com