BENPOL – GOOD BOY ALIYE CHANGANYIKIWA Benpol ft Darassa tatu

Pamoja na kuwa mkali wa RnB, Benpol pia preasure ya Show biz haimuachi. Wiki ya tatu ya mwezi May 2017 aliweka picha ambazo zilimuonesha akiwa uchi kwenye mtandao wa Instagram. Picha zilizowakera wapenzi wengi wa muziki wake, ambao walitoa maneno mengi kumkashifu na wengine kuonesha masikitiko yao, kwani hawakuwa wanamuona Ben Paul kama msanii wa kupost picha hizo.

Baada ya siku chache BenPol leo ametoa wimbo mkali alioupa jina la #3… ambao bado kwa maoni yangu bado sikuamini maneno BenPol ameimba.

“Tako tatu wazungu waaah” ni lugha ya mtaani jijini Dar es salaam ambayo ina maanisha, mwanaume kufanya mapenzi kwa muda mfupi tu na ku-enjaculate au kuingiza uume mara tatu tu na kurusha “wazungu” ambazo ni sperm.

Hii lugha inaweza kuwa imetumika tu hapa ikiwa imebeba maana nyingine lakini hiyo ndio maana yake ya moja kwa moja. Lakini kabla hatujamuhukumu Benpol, sioni kama amekosea chochote.

Show business au kwa kifupi showbiz, ni neno maarufu sana tangu miaka ya 1850 ambapo limekuwa likijuisha aspects zote zinazofanyika katika soko la burudani (Entertainment industry) Show biz. Kwa kipindi kirefu sasa tangu burudani igeuzwe kuwa kazi, vijana wengi hasa wanamuziki eg. AY, Jose Chamilion etc… walishika usukani wakishirikiana na wadau wengine muhimu, na hatimaye matunda yameanza kuonekana.

Hivi karibuni tumeona vijana wengi Afrika Mashariki wakitajirika kupitia muziki mfano Sauti Sol, Diamond, Alikiba na wengine wengi… teknolojia imefungua mipaka na sasa imekuwa rahisi wasanii kusambaza kazi zao. Jambo hili limeweka presure kwa wasanii kufanya vizuri.

Hivi sasa msanii ana kazi ngumu zaidi ya kufanya muziki wake kuwa biashara, japokuwa soko limefunguka zaidi. Msanii hatoi mziki mzuri pekee, bali analazimika kuwa na timu nzuri nyuma yake ili kuweza kusimamia kazi zake na kufanya marketing kwa ajili ya kuupatia soko muziki huo.

Kila msanii anafanya kazi nzuri na wengi pia wanatumia mbinu na channel zinazofanana ili kuwafikia watumiaji.

Radio: Inatakiwa msanii awe na contacts za kutosha na influence hasa kwenye media kubwa ikiwa anataka kupata prime time interviews. Wasanii wengi wakubwa wana – Premier ngoma zao kwenye show kubwa kama XXL Clouds FM ya @Bdoze, Plannet Bongo East africa radio ya @Dulla au Mashariki mix ya the Citizen radio kwa mzee mzima Willy Mtuva na show nyingine kubwa Afrika mashariki ambazo ziko na foleni ya wasanii.

The same kwenye TV shows kubwa, unakuta kuna msururu wa wasanii ambao wanataka kupata nafasi ya kuwa kwenye interview… lakini cha msingi hapa ni je unapataje nafasi wewe na si mwenzako?

Msanii thamani yako inatokana na followers ulio nao na kiasi gani mtandao unakuzungumzia.

Hii imepelekea wasanii kuja na mbinu tofauti za kufanya marketing stunt za kuwafanya wapenzi wa muziki wamzungumziewakati mwingine bila kujali maadili ya stunt hizo… Diamond Platnumz anajulikana kwa kufanya stunt kubwa kubwa mfano wakati ameonekana na mama watoto wake kwa mara ya kwanza kabisa alisema ile ilikuwa project, but tunajua kilichoendelea kwenye uhusiano wao… wapo pia wasanii kama Willy Paul ambaye aliwapa kichaa mashabiki alipoweka picha zake za harusi na Alaine. na baadae akatoa ngoma na mwanadada huyo.

Cha kufanya tufurahie muziki wa wasanii wetu na kuwaunga mkono maana ubunifu sio kitu kirahisi. Wapo watakaoteleza kidogo na tunapaswa kuwakumbusha ili tuendelee kufurahia “Tako tatu wazungu waaah”

BENPOL – GOOD BOY ALIYECHANGANYIKIWA Benpol ft Darassa tatu

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com