NAKAAYA SUMARI ALLAN LUCKY WAONEKANA KIWANJA

Kiwanja hiki kipya mjini hapa ndio kinachovutia watu wengi wanaotaka kula bata na kuku kwa wakati mmoja. Kipo mbele kidogo ya round about ya kuelekea Arusha. Siku ambazo zinahappen sana hapa kwa mujibu wa Mnyatiaji ni siku za jumatano mpaka jumapili.

Anaitwa Socrates Mtoba, mtaalamu wa mawasiliano mtandaoni. Hapa anamimina JUICE huku kazi inaendelea.
Design kama sanaa pia imehusika vizuri katika kuhakikisha hii area inakuwa ya kuvutia to the maximum.
Kuna Ka-stage ka kishkaji kwa mbaali unakaona.

Zipo counter tatu. Ya chakula, ya kahawa na chai, na nyingine ya ndio ilee unayoiona hapo ambayo ni ndio ina vilevi na mavitu ya kikubwa.
Vijana wa kisasa wasiotumia kilevi wanapata juice amazing. Emmanuel Florid mtaalamu wa maswala ya usambazaji wa bidhaa mbalimbali amem-minya mrembo huyu vizuri. Strickly Tanzanian, nimependa hiyo kacha aliyovaa mkononi.

Nilikuwa nataka kuzungumzia hii juice na jinsi ilivyokuwa tamu kwa sababu Sistaree… Nakaaya Sumari alikuwa kama hataki kufotolewa. Siku hizi kama ulikuwa unajiuliza yuko wapi hasikiki akitoa ngoma mpya na vitu ka hivyo, basi ujue amefocus kwenye kuendesha kampuni yake ya events organzing. Hapa alikuwa anarekebisha mipango.

Endelea kufuatilia michapo ya watupipo.com kwa mapicha picha kibao na stori za kitaa.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com