STEFANO BOERI NDIYE AME-DESIGN JIJI LA MSITU CHINA

Wakati ambapo umeanza kuhisi kwamba hii ni post ya nyumba kali za kusadikika, naomba nikujulishe hii ni habari fupi kuhusu kazi nzuri inayofanywa na mbunifu majengo mwenye kipaji cha hali ya juu duniani anayeitwa Stefano Boeri raia wa Italia.

Moja kati ya vitu vinavyofurahisha zaidi kuhusu Stefano ni kwamba, ni mtu anayejali sana mazingira na ukaingalia kazi zake nyingi zinaonesha hivyo.

Hivi sasa stori kubwa zaidi nchini China kuhusu miundombinu ni kupitishwa kwa mpango wa ujenzi wa Jiji la msitu. 

Hili ni jiji ambalo litakuwa limeoteshwa miti 40,000 na mimea mingine milioni moja, linatazamiwa kumalizika mwaka 2020. Pamoja na kwamba China ni moja ya wazalishaji wakubwa sana wa C02, serikali ya nchi hiyo imekuwa mstari wa mbele pia kutafuta solutions. 

Jiji hili linalojengwa Kaskazini mwa Liuzhou litakuwa na uwezo wa kuishi watu 30,000 huku likikusanya kiwango cha C02 cha tani 10,000 na kuzalisha Oxygen kiasi cha 900 tani. Miji kama hii inahitajika sana ili kuitunza dunia yetu hii kwa vizazi vijavyo.

Once completed, the new city will host 30,000 people, absorb almost 10,000 tons of CO2 and 57 tons of pollutants per year and produce approximately 900 tons of oxygen.

Imeletwa kwako na #Itunze Read more about China wants to build a forest city to tackle air pollution 

Picha zaidi za kazi alizowahi kufanya Boeri.

Asante kwa kupitia watupipo.com karibu tena mazuri yanakuja.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com