MAKAMBA: NITASIMAMIA TURUDISHE UHAI KATIKA MTO RUAHA

“Hii sio picha nzuri” ameanza kusema January makamba ambaye ni waziri mwenye dhamana ya mazingira nchini Tanzania. Nimesimama ndani ya tumbo la mto Ruaha uliokauka. Kabla mwaka 1993 hakuna aliyewahi kuona ndani ya mto huu kwani haukuwahi kukauka hata mara mmoja. Wakati inaweza kuonekana sio kitu kwa sasa, kuna sababu ya msingi ilifanya mto huu kupewa jina na cheo cha la GREAT.

(kama ilivyokuwa kwa marehemu Kanumba the Great) – Huu ni mto mkubwa mpana uliojaa maisha. Wanyama aina mbalimbali kuanzia Kiboko, Mamba, Tembo na wanyama kwa mamilioni… Ndege wameruka kutoka Ulaya mpaka kwenye mto huu ambao kitako chake kina upana wa km 85,000 za mraba, kubwa zaidi ya Rwanda, Burundi, Comoros, na Swaziland na Gambia zikijumuishwa. Kwa sasa asilimia 70 ya umeme wa Tanzania unatokana na mto huu.

Kiasi kikubwa cha kilimo cha umwagiliaji kinatokana na mto huu, mfano wa karibu ni kilimo cha miwa Kilombero ambacho kimezalisha mabilioni ya pesa kinatokana na uhai wa mto huu… Uduzungwa forest ambayo ina wanyama adimu zaidi duniani na pia asilimia 10 ya Simba waliobakia duniani wanategemea maisha ya mto huu pamoja na ukijani katika Rufiji Delta.

Mwaka jana nilitembelea mto Ruaha, kuanzia chini kabisa mpaka juu ambapo mto Rufijii unaringishia kona zake nzuri, nimepitia Kilombero, mbuga za Ruaha, Kilolo, Mbarali mpaka Uswangu mpaka milima ya Kipengere mpaka Kitulo national park Makete.

Hapa niliposimama hakuna binadamu aliwahi kufikiri atasimama, Leo hii ukikatiza katika mto huu utakutana na Viboko, na Mamba wakijaribu kujipooza kwenye matope ambayo yamekosa Oxygen, na ni kitu cha kawaida kukuta mzoga wa Kiboko pembeni huku Voltures wakizunguka kupata mlo kutokana na mizoga hii huku ukikaribishwa na hafuru kali ya shombo ya samaki waliokufa. Sio kitu kizuri kuona nature ikifa kama hivi. Hali hii inatishia sana uhai wa maisha ya binadamu.

Tunachokifanya kwa sasa kutokana na hali hii… Kwanza naomba niseme uwazi kwamba tutarudisha mto Ruaha uweze ku-flow kwa mwaka mzima tena. Hii itachukua kazi kubwa sana na ninashukuru sapoti tunayoipata kutoka kwenye ngazi za juu kabisa za serikali zaidi makamu wa rais Samia Suluhu ambaye amekuwa mstari wa mbele kusapoti jitihada hizi.

Nilipotembelea Katavi tulifanikiwa kurudisha uhai wa mto Katuma na sasa unaendelea kusaidia uhai. Tumeanza kushuhulikia mkakati maalum na hatutakubali jitihada hafifu za kawaida katika kufanikisha hili. Tunategemea jitihada kutoka kwa watu na taasisi zote zenye interest na mazingira, tunashukuru Benki ya dunia kwa kuonesha nia ya kufanya kazi na sisi katika eneo la umwagiliaji wa kisasa katika mto huu…

Mtembelee ukurasa wa January Makamba kwa update za karibu zaidi katika jitihada zake za kurudisha mazingira katika uhai wake. Watupipo.com itaendelea kufuatilia jitihada za Africa mashariki katika uhifadhi wa mazingira kwa karibu pamoja na ku kutambua mchango wa teknolojia katika kuhifadhi mazingira. Tembelea Itunze uweze kujiunga na kuwa sehemu ya movement ya uhifadhi wa dunia yetu

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com