WATEJA 63,000 WAMEKATIZA ORDER ZAO ZA GARI INAYOTUMIA UMEME “TESLA MODEL 3”

Wateja 63,000 waliokuwa wameweka order ya kutengenezewa gariya Tesla model 3 wamekatisha order zao according to CEO wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Tesla Elon Musk.

Katika mazungumzo Musk amesema kwamba kampuni yake ilipokea order zaidi ya 518,000 lakini mpaka sasa wamebakiwa na order 455,000.

Katika maelezo yake Elon Musk amesema kwamba hilo sio tatizo kwa sababu order walizonazo mpaka sasa zitawafanya wawe bize kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo. Amesema (mfano) huwezi ukawa na restaurant ambayo ina order za kutengeneza burger kwa zaidi ya saa moja na nusu halafu ukaendelea kuwaambia watu waweke order.

Hata hivyo Tesla imesema wale ambao bado wanaweka order za gari hii ya Tesla Model 3, watapata gari zao angalau kuanzia mwisho wa mwaka 2018.

Mwaka huu kwa mara ya kwanza katika historia ya magari ya umeme duniani Tesla inaanza kuzalisha Magari yake kwa ajili ya soko la daraja la kati ambapo Elon Musk aliwaambia wafanyakazi wa kampuni hiyo kwamba wanaingia kwenye production hell kwani wanahitaji kuzalisha magari mengi kwa ajili ya wateja wao.

Tesla ina mpango wa kuzalisha magari 5000 kwa wiki Ifikapo mwezi Dec 2017 na kufikia mwaka 2018 mwishoni itakuwa ikizalisha magari 10,000 kwa mwaka.

Pamoja na kupost hasara katika robo ya pili ya mwaka wa biashara, Tesla imetajwa kuwa na thamani zaidi ya kampuni za magari za General Motors na Ford yote ya nchini Marekani.

WATEJA 63,000 WAMEKATIZA ORDER ZAO ZA GARI INAYOTUMIA UMEME “TESLA MODEL 3”

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com