BABA YOWERI MUSEVENI ANATUAMBIA “TUZALISHE NA KUTUMIA BIDHAA ZETU WENYEWE”

Moja kati ya vitu vinavyoashiria uchumi wa taifa fulani ni pamoja na bidhaa zinazozalishwa katika taifa hilo. Hapa Afrika mashariki nchi zetu bado uchumi waetu bado unachipukia na suala la kuagiza bidhaa za Ulaya na Asia kwa ajili ya matumizi muhimu uko juu sana.

Rais wa Uganda HE Yoweri Museveni katika uzinduzi wake wa Uganda oil pipeline nchini Tanzania ametukumbusha wananchi wa Afrika mashariki kutumia vitu tunavyovitengeneza wenyewe. Alisema kwamba hivi sasa Uganda inaanza kuzalisha mafuta ya aina tofauti kuanzia mafuta ya ndege, ya magari na mitambo kitu kitakachopunguza bei ya mafuta nchini Uganda na Afrika mashariki kwa ujumla.

Seriously, uzalishaji  huu wa mafuta ambayo ni bidhaa muhimu sana kwa maendeleo ya Afrika mashariki ni hatua muhimu sana kwetu, hivi sasa hapa nchini Kenya bei ya petroli lita moja ni Sh 95 mpaka 100 na kuendelea wakati mwingine, huku nchini Tanzania mafuta hayo ni Sh 1995 mpaka 2000 na kuendelea wakati mwingine.

Hii inafanya kila kitu kinakuwa kigumu kwa mwananchi wa kawaida kuanzia bei ya chakula mpaka bei ya nauli ya Matatu au daladala kwenda kazini. Wakulima wanaotumia mafuta kumwagilia au kuandaa mashamba nao wanajikuta wakitumia pesa nyingi kwenye gharama za matrekta na umwagiliaji, mwisho wa siku hata kilimo cha kisasa wakati mwingine kinakuwa kigumu kufanyika.

Lakini kikubwa nilichokipata kwenye kauli hii ya Museveni ni kwamba, sio kwa upande wa mafuta pekee bali bidhaa muhimu pia kama chakula kizalishwe hapa nyumbani. Ni aibu sana nchi hapa Kenya tushindwe kufanya kilimo cha kisasa kiasi cha kuweza kustahimili ugali wa nchi nzima na pengine kusaidia nchi kama somalia, na ni kitu cha kushangaza Tanzania kuzuia mahindi kwenda Kenya kwa kuwa bado hayatoshi kulisha wananchi wake yenyewe.

Kifupi ni aibu kwa nchi Ukanda wa Afrika mashariki kununua bidhaa kama mahindi kutoka nje ya Afrika, na bidhaa zinginie kama nguo. Hivi sasa kuna takribani wananchi milliomi 200 Afrika Mashariki yote, na hili ni soko la uhakika kwa wajasiriamali na wazalishaji wa bidhaa muhimu.

Yoweri Museveni ametukumbusha pia sisi watumiaji wa bidhaa, kwamba tutumie bidhaa zinazozalishwa hapa nyumbani ili kuwawezesha wazalishaji wa bidhaa hizi kukua. Hivi sasa East Africa Community inachomoza na zipo opportunity nyingi ssana za ajira kwa vijana wenye nguvu za kulisha ukanda wetu huu, kwa nini tusizichukue fursa hizo?

Asante kwa kupitia watupipo.com tutaendelea kukusogezea habari za watu wa Africa Mashariki na mbinu za kuwekeza kutoka kwa wataalamu, na pia challenges zinazowakuta vijana wanaokimbizana na uwekezaji hapa Afrika mashariki.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com