HIZI NDIO COST ZA KUWA MAPENZINI NA CELEBRITY

Mapenzi na mtu maarufu wakati wewe sio maarufu yanaweza kuwa dangerous sana. Ni miujiza tu ya Mungu inatakiwa ikupe nguvu ya kuvumilia vitu vingi wanavyofanya na aina ya maisha anayoishi mtu maarufu. Kitu cha kwanza hutakiwi kabisa kuwa na wivu hata chembe mwilini mwako, na pia hutakiwi kuwa na masharti mengi la sivyo uhusiano utauona ukitokea dirishani na hutakuwa na cha kufanya.

Boys na girls (mimi inlcuded) tumewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu maarufu kwa namna moja au nyingine, haijalishi ilikuwa serious au Bang bang relationship lakini experiences nyingi huwa ni za maumivu kwa upande mmoja. Na ndio maana nakuambia kama hujadate Star usijaribu kwa lengo la kudumu mahusianoni.

Kitu cha kwanza ni ratiba ngumu za kazi;

Hapa nituzungumzia wasanii wa muziki kwanza, ambao wako aina tofauti lakini hapa nitafocus kwa hard working na lazy ones. Ratiba za msanii ambaye ni hardworking na yuko comited kwenye kazi yake huwa ni ratiba ngumu sana kuweza kumfurahisha mpenzi. Huyu ataamka kuanzia saa 6am mpaka kitu 9am hapo akiwa tayari na meetings na sessions za mazoezi.

Sanaa ikiwa kazi inahitaji kufanyiwa mazoezi karibu kila siku ili kuweza kuwa juu. Hizi ni baadhi tu ya meetings ambazo unaweza kuzisikia; Kukutana na managers, choreographer, photo shoot, interviews (na hizi huwa mbaya zaidi wakati wanapofanya media tours) meetings na makampuni kwa ajili ya endorsements na biashara nyingine meetings na promoters yaani ni meetings meetings na kama hakuna meetings kuna studio sessions za kumwaga.

Kwa boyfriend anayetegemea kupata lunch na bae au dinner na bae kila siku hii huwa ni ngumu zaidi ya chuma.

Kwa upande wa msanii ambaye hayuko serious sana na sanaa yake, huwa ratiba zake ni laini kidogo na hizi zinategemeana kiasi gani ana-chill na marafiki, Studio sessions, mara kadhaa kwa mwezi atakuwa na meetings na promoters na choreographers, huku photoshoot pia zikiwa kadha kila mwezi, pamoja na media tours.

Hapo wote sijazungumzia suala la shows na performances za wasanii hawa ambazo huwa zinaunganisha safari na late hours karibu kila weekend.

Kitu cha pili hapa ni ishu ya wivu.

Kitu kikubwa ambacho kilikuwa ni challenge wakati natoka kisirisiri na mrembo flani kwenye game ya Bongo flava ilikuwa ni jinsi anayodeal na wanaume wengine wanaomzunguka. Msanii kama unavyojua anachukua attention ya watu wengi na kujulikana kwake kunakufanya wewe uwe na wapinzani wengi zaidi, nadhani hata wakati niko nae nilikuwa kama side nigga tu maana mara nyingi alikuwa na vijeba wengine.

Msanii atakuhakikishia mkiwa chumbani kwamba wewe tu ndio uko nae lakini kwa mavazi na ratiba za usiku pamoja na escort za wanaume kumrudisha nyumbani nyakati za usiku mnene, hazivumiliki. Sio kila msanii anafanya usaliti katika mapenzi lakini kwa wewe ambae ndio mpenzi wake lazima tabia yake itakuchosha na utanyanyua kilicho chako na kutafuta wa size yako.

Yapo mengi sana ambayo yatakufanya ushindwe kudate mtu maarufu na hasa msanii, na ndio maana mapenzi mengi huwa hayadumu. watupipo.com inakaribisha povu lako kama umeshawahi kudate au una lolote la kuchangia kwenye stori hii. Au kama una sori yako ungana na sisi kwenye ukurasa wetu wa Facebook watupipo.com utupe mchapo wako.

Photo credit : Ngaz kwa ngaz

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com