VITU SABA VITAFUATA FURAHA YAKO, SUCCESS IS ONE OF THEM

Tunakubaliana sote kwamba maisha huja mara moja na kuondoka mara moja, hukujipangia kuzaliwa na pia hutajipangia kufa. Lakini kuna vitu unaweza kujipangia wakati huu wa uhai na afya yako. Ingawa ukakasi wa hali ya maisha na masaibu mengine huwa vikwazo.

Njaa, maradhi, pesa na vingine hutusababisha tuujisahau na kupoteza raha ya maisha. Asubuhi na mapema unakutana na watu wamenuna wakielekea kazini wengine wamelala late jana yake so wanasinzia kwenye gari huku Konda/Deree wakiwa na kauli chafu na inaendelea hivyo mpaka kwa CEO wa kampuni unayoifanyia kazi… kila unapogeuka unakutana na negativity kiasi kwamba unajikuta na wewe umeambukizwa.

Je unawezaje kubadilisha hali hii na uwe na happy all the time? How can we be happier everyday? How can we create our own happiness and that if the others?

Hizi point chache zikusukume kuanza kutafuta furaha yako kutokan ndani yako na uweze kuwaambukiza wengine.

YOLO: you only live once na hakunaga marudio kila siku ni kusoga mbele. Kile ambacho ulikifanya jana na hakikuwa vile ulitarajia, leo uko kufanya vizuri zaidi bila kuona kwamba jana ulishindiwa pale na hutaweza tena. Uwepo wako siku ya leo ni wa kusherehekewa kila wakati.

Ukiwa happy, mambo haya yatakufuata kama upepo wa jangwa la Kandahar.

UTAJIAMINI ZAIDI na uwezo wako kukamilisha kila unachokiwekea akili, nia na focus yako.

MAHUSIANO yako utayaweka kwenye kilo ya nani anakuheshimu na kukupenda kwa dhati na utaachana na wale wanaokuchukulia poa.

PITA PITA zako na interactions na watu wengine zitakuwa za kijiamini na hutatishika au kujiskia intimidated mtu kutokana na kazi anayoifanya au mafanikio yake. Hutapoteza muda wako kujilinganisha na wengine, coz unaamini kuwa safari yako ni tofauti na zao.

UNACHAPA KAZI zaidi kwa motivation unayojipatia bila kufikiria approval za watu wengine. Mafanikio huja namna hii na sio vinginevyo.

CHALLENGES HAZIKUTISHI tena maana tayari unajiamini kuwa wewe uko na njia ya kutafuta suluhisho katika kila kinachokuface… Huhitaji jeshi la nje.

MANENO ya watu hayatakusumbua kwa sababu tayari unajua wewe ni mtu wa aina gani na unajikubali hivyo ulivyo.

NI NGUMU kukuangusha kwa vile umeshajizoesha kusikiliza nafsi yako na kupata sapoti ya wale wenye nia njema na wewe. Utakuwa tayari kujitetea na misimamo yako popote pale.

VITU VIZURI huanza kukufuata na hasa vile unavyoviombea na kuvifanyia kazi hutokea. Universe energy hufanikisha pale unapokuwa katika mkao wa kupokea.

YOLO au kwa kirefu You Only Live Once, ni statement maarufu miongoni mwa vijana wa kisasa na hasa wale wanaogonga yai (wanaozungumza english) ikiwa na maana; “Una nafasi moja tu ya kuishi” Mara nyingi vijana wamekuwa wakitumia maana hii kufanya maamuzi tofauti na wakati mwingine kujifariji kutokana na maamuzi mabaya au mazuri waliyofanya… But hii sio maana yangu kuandika hii article fupi Jumapili ya leo.

Asante kwa kutembelea na kusoma watupipo.com niandikie kama una lolote unataka kuongeza kwenye article hii watupipo.com@gmail.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com