UTAFITI : KAMA AME-CHEAT MARA MOJA ATARUDIA TENA. Mambo 4 yanayotokea katika usaliti

Unapokuwa katika uhusiano na mtu halafu akaku-cheat utamuamini kwamba hawezi kurudia? Katika study iliyofanywa na chuo kikuu cha Denver imeonesha mtu aliyewahi kusaliti katika uhusiano ni rahisi kurudia tena.

  1. Utafiti

Katika study iyo ambayo ilihusisha watu 484 huku asilimia 68 kati yao wakiwa ni wanawake. Kila mtu alitakiwa kujibu angalau maswali mawili kuhusu mahusiano. Imagine asilimia 44 kati ya hao wali-report kula tunda nje ya mahusiano yao.

Asilimia 30 kati ya watu hao wali-report kwamba partners zao wali-cheat.

Fast forward; watafiti walifanikiwa kugundua kwamba mtu aliyewahi kucheat before (iwe kwenye uhusiano wa sasa au ule wa zamani) – uwezekano wake wa kufanya tena ni mara tatu zaidi ya yule ambaye hajawahi ku-cheat.

  1. Msalitiwa kuwa msaliti

Usaliti hauwaachi salama wale ambao wamefanyiwa kamchezo kachafu, kwa sababu watafiti waligundua kuwa wale ambao walisalitiwa before (either katika uhusiano wa sasa au ule wa zamani) na wao uwezekano wa ku-cheat unakuwa mara mbili zaidi ya wale ambao hawajawahi kusalitiwa.

“So hapa utaona vile mabazazi wanavyowaharibu kondoo wasafi wa bwana”

  1. Je cheater hawezi kubadilika?

Ingawa ni kweli kwamba mtu aliyewahi kusaliti anaweza kurudia tena, haimaanishi kwamba ni lazima atarudia. Tafiti imeonesha asilimia kubwa ya watuwaliowahi kuchafua mahusiano yao yaliyopita wakijirekebisha na kuwa waaminifu kabisa.

  1. Ufanye nini ili asirudie?

Pengine jibu rahisi ni – Kuachana nae – Lakini kama ni vigumu kumuacha, mtaalamu wa saikolojia Frank Dattilio anasema ikiwa mpenzi wako amekusaliti na umegundua. Fanya jitihada pindi unapokuwa tayari, mzungumzie usaliti huo vizuri.

Tumia akili yako na sio emotions kumuangalia ikiwa kweli anajutia usaliti huo au anaonekana kutokujali.

Usipozungumza naye vizuri ukajua mazingira na sababu zilizomfanya akuchafulie kitumbua chako, kuna uwezekano mkubwa sana wa kurudia.

Lakini kama hajali na anasema tu sitarudia… Mpuuzi huyo atarudia tu. Tupa kule akafie mbele.

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com