WEWE MWENYEWE NDIO UMEJIFIKISHA KATIKA MAISHA ULIYONAYO…Hatua hiyo haitoshi.

Hii story itakufanya ujisikie vibaya, lakini itakujenga.

Ni makosa kuwa na upeo, mpenda watu, kuelimika kuwa, kuwa intelligent, na degree 1 au 2, wakati bank account yako inachechemea – Edmund Jim.

Kuna watu wanaona ni afadhali kutafuta kazi kwa miaka 2, 3, mpaka 5 na wasione shida yoyote. Wanaona kuanzisha biashara ni kitu kigumu sana. Unakuta mtu anafanya kazi miaka 25 au 35 na bado anastaafu akiwa amechapa mfukoni. Hiki pia, ni kitu kawaida ya maisha.

Mi naona ni afadhali nifanye kitu kigumu, ili kupata pesa, itakayonisaidia baada ya kustaafu. Badala ya kufanya kitu kirahisi, then nije kuteseka bila pesa ninapostaafu. Nchi hii inaongoza kwa kuwaharibu wale wenye upeo, na kuzawadia wasio na upeo. Na sababu haiko mbali.

Watu aliosoma na wenye upeo, wana hofu. Wana uoga kwamba vitu vinaweza visifanikiwe au kuharibika. Hivyo wanakuwa makini kupitiliza ili wasiharibu. Wanataka kujua kila kitu kabla ya kutenda chochote. Hivyo unakuta muda unakwenda bila kutekeleza na wanafeli.

Lakini mtu asiye na upeo, hutenda bila upeo.  Wanafanya actions za kijinga kwa confidence, hata kama hawajui details. Wanajikuta wakijifunza huku wanakwenda. Wanachukua risk kubwa na mwisho wanafanikiwa.

Watu hawa. Hawajiwekei mipaka kama ambavyo, wenye upeo hufanya. Watu wasiojua hufanya makosa mengi, na wakati wanavyokosea ndio wanazidi kujifunza, na kufanya mazoezi na siku moja mgodi unatema wanafanikiwa.

“Hivyo, hii ni ishu ya emotion zaidi”

Sio kwa ubaya. Shule zinatukataza kufanya makosa, au kufeli. Hilo ndio kosa kubwa la shule. Lakini maisha yanakufundisha kufanya mistakes, ili ujifunze na kukua.

Hakuna anayeweza kufanikiwa bila kufanya makosa, hivyo kama unaogopa kufeli tayari umeshafeli.

Mafanikio yanakwenda kwa wale wanao yawazia. Na kufeli kunakwenda kwa yule anayekuwazia. Napoleon Hill, author Think And Grow Rich.

Ndio maana kuna watu wengi wanaojua, wenye upeo na hawana mali. Wako vizuri kichwani, lakini moyoni hawana kitu.

“Nimegundua kitu kingine, wakimbiaji kwa kasi hawashindi marathon. Na wajasiri hawashindi mapigano.

Wenye busara siku zote hawapati maisha. Wenye akili hawapati utajiri. Na watu wenye uwezo, hawafiki position za juu.

“Bahati mbaya hutokea kwa kila mmoja”

Kitu kingine kinachowafelisha watu wenye upeo ni EGO. Hawaonagi umuhimu wa kuuliza wajulishwe, huwa wana majivuno ya upeo.

Nakuhakikishia ukijishusha kidogo. Ukauliza kwa unyenyekevu na ufanyie kazi information unazozipata kwa ushupavu. Utawashinda wengi hata walioanza kabla yako.

Elimu ikichanganyika na ubinadamu ndani ya mchapa kazi, huleta matokeo ambayo kila mtu atashangaa.

Mentor wangu husema “Ni kile ulichochagua ndio kimekufikisha hapo ulipo, nina hakika bado ni chini sana” Fikiria huu msemo, Una nguvu ajabu.

Maisha yako yaliyopita yamekufikisha ulipo sasa. Lazima ufanye maamuzi ya kusahau na kuanza upya kujijenga zaidi.

Leo nawashauri weye elimu wenzangu, tafuta na utapata, gonga utafunguliwa mlango, na omba utapewa.

Kuwa tajiri ni ngumu na kuwa maskini ni ngumu zaidi, chagua wewe, je ni ngumu ipi unataka kukabiliana nayo?

Writter: Unknown

Source: Whatsapp.com

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com