TUNDU LISSU KAGOMEWA KAMA ALIVYOGOMEWA RAILA ODINGA…Je hii ina maanisha wafuasi wamegoma kufuata kila wanachoambiwa?

Kitendo cha wafuasi kugomea maelekezo ya kiongozi, sio kitu cha ajabu. Siku za hivi karibuni, kitendo hiki kimezidi kuwa maarufu.  Sio kwenye siasa tu hata katika jumuia za sheria pia migomo ipo. Ingawa sisemi ni kwa nia mbaya.

Hivi juzi tar 27 August. Rais wa chama cha wanasheria nchini Tanzania Tundu Lisu, aliwaomba wanachama wa chama hicho, kugomba kwenda mahakamani na kwenye mabaraza ya sheria.

Lisu alisema hii ni namna ya kuonesha solidarity juu ya kitendo cha kulipuliwa kwa ofisi za wenzao wa IMMMA Advocates jijini Dar.

“Half of the troubles of this life can be traced to saying yes too quickly and not saying no soon enough.” –  Josh Billings

“Nusu ya matatizo ya maisha yanasababishwa na kusema ndio haraka na sio kusema hapana haraka zaidi” –  Josh Billings

Katika tamko lake kwa waandishi wa habari, Lissu akiwa ameongozana na viongozi wa juu wa TLS alisoma tamko hilo lililofanywa na uongozi wa juu wa chama cha mawakili na kusema.

Kitendo cha kugoma kitawafundisha waliofanya tukioo hili kuona umoja wetu ili wasiirudie tena kufanya hivi.

Baadhi ya vijana waliozungumza na watupipo.com, wameonesha kusikitishwa na uamuzi huu wa TLS na kusema kuwa kitendo hiki kingesababisha wateja wao wapate shida.

Wakili wa kujitegemea na Mkurugenzi wa Smile Attorneys, Leonard Manyama, amepinga agizo hili na kusema hawezi kugoma siku ya jumanne wala jumatano kwa kuwa itakuwa ni adhabu kwa wateja wake.

Hii sio mara ya kwanza kwa wanaoongozwa kupinga wazi maamuzi ya viongozi. Huku wakitoa sababu zenye mantiki kwa kupinga kwao.

Nchini Kenya wananchi pia waliamua kumgomea Raila Odinga, aliyekuwa mgombea uraisi wa NASA. Odinga aliwataka wafuasi wake kutokwenda kazini siku ya jumatatu.

Raila alitaka wananchi kuomboleza mauaji ya (waandamanaji) waliokuwa wafuasi wake, huku wakisubiria tamko lake kuhusu kupinga matokeo yaliyokuwa yametangazwa na IEBC.

“We need to learn the slow ‘yes’ and the quick ‘no”- Tom Friel 

“Tunapaswa kujifunza ndio ya taratibu na hapana ya haraka” – Tom Friel

Baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii walionesha kupigwa na sintofahamu kwamba ikiwa hawataenda kazini je nani atawanunulia chakula?

 

Je hii inaonesha demokrasia au ni kwamba baadhi ya viongozi wanaomba zaidi kwa wafuasi wao na kushindwa kusahau maisha yao?

Nini maoni yako juu ya matukio haya mawili?

 

 

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com