ALICHOKIFANYA RAIS KAGAME, KWENYE CONFERENCE YA TED GLOBAL TANZANIA…Amesema yeye hufanya maamuzi kutumia moyo na akili.

Rais Paul Kagame wa Rwanda amekuwa mmoja kati ya wazungumzaji kwenye kongamano la TED linaloendelea jijini Arusha Tanzania. Kagame hakuweza kufika kwenye kongamano hilo lakini amezungumza kutumia Skype akiwa Kigali.

“Muwe wakweli” amesema Kagame akiwaambia waandishi wa habari kuhakikisha wanasema ukweli kwenye ripoti zao na kuwaachia audience kufanya judgement.

Kagame ni mmoja kati ya Marais wachache Africa ambao wanawekwa kwenye kundi la Innovators, na amekuwa akisifiwa kwa kufanya mapinduzi makubwa nchini Rwanda katika kipindi cha utawala wake.

Katika interview aliyofanyiwa na mwandishi kutoka Zimbabwe Vimbaye Kajase, Rais kagame alijibu maswali kuhusu familia yake na kazi, huku akisema anapenda kufanya kazi na watu wakweli.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni

Vimbayi : “Unaweza kusema unafanya mamuzi mengi kufuata moyo wako au akili”

Kagame : “Vyote”

Vimbayi : “Una-sound kama mtu anayetumia akili”

Kagame pia ameweka wazi kuwa, hawezagi kuweka ahadi ambayo anajua hawezi kuitimiza.

Kitu ambacho wengi hatukifahamu kuhusu Kagame ni kwamba ameanza ku-tweet kabla hata ya rais wa Marekani Donuld Trump.

Mwaka huu rais Paul Kagame alichaguliwa tena kushika urais kwa asilimia 99.

Kongamano hili linafanyika kwa mara ya pili nchini Tanzania katika jiji la kitalii la Arusha, huku mara ya kwanza ikiwa miaka 10 iliyopita.

watupipo.com inaendelea kukuleta yanayoendelea katika kongamano la TED.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com