ABORT ABORT, KUMBE WALE WEZI WA GARI MOMBASA WALIKUWA FEKI…Polisi inawashikilia waganga na mwenye gari.

Kwa mshangao mkubwa nimekutana na habari kwamba… Habari zilizovuma sana leo za wale jamaa waliokuwa wakicheza uchi kwa maelezo kuwa wameiba gari na kulogwa imegundulika kwamba lilikuwa ni tukio feki.

Polisi mjini Mombasa wametoa tamko la kuwashikilia watu hao, pamoja na waganga wawili na mama mmiliki wa gari iliyokuwa ikinyweshewa maji. (poor car)

Swali kubwa ambalo sijalipatia majibu ni je, maisha yamekuwa magumu kiasi hichi jamani?

Inafikia wakati mwanaume na nguvu zake anafanyishwa udhalilishaji wa aina ile kwa kutafuta kiki tu?

Jamaa ukiangalia picha zao unaona jinsi walivyokuwa busy kubinua makalio yao meusi mele ya hadhara, huku wakionesha kweli kwamba wamechizi… kumbe ni tukio feki la kupangwa?

Wapo watu wanaoamka kila siku na kufanya biashara haramu lakini kitendo cha kuvua nguo na kutembeza maumbile ya mwanaume mbele ya kila mamia ya raia walikuwa pale pamoja na mamilioni tuliotazama mtandaoni, ni kitendo cha kigaidi kabisa.

Anyways ningeweza kusema zaidi juu ya hili tukio lakini haina maana. Vijana inabidi tutafute pesa kwa jasho halali na sio kuingiza watu kingi kama hivi.

Waganga hao wanaoshikiliwa na polisi huko Mombasa wamewashtaki pia kwa kukutwa na nyoka, bila kibali hivyo wameshtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Stori hii pia iliandikwa na watupipo.com itazame since sasa unajua kwamba hili ni tukio feki.

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com