MAMBO HAYA 5 YATAUA KABISA UCHUMI WA VIWANDA TANZANIA…Unless yafanyiwe kazi chap chap.

Waswahili wanasema  usipoziba ufa, utajenga ukuta. Nyumba imara itajengwa kwa msingi imara.

Chukua misemo hii uiweke kwenye elimu ya Tanzania, hasa wakati ambao nchi inalenga uchumi wa viwanda.

Tangu kupata uhuru, mitaaala ya elimu imekuwa ikibadilika kuendana na sera ya elimu, na uhitaji mkubwa wa soko kwa wakati huo.

Serikali ya awamu ya tano, inataka kuhakikisha Tanzania inajenga uchumi wa viwanda na kujisogeza mpaka kwenye uchumi wa kati.

Ni nia nzuri, lakini je tutaweza?

Robert Herjavec alisema “Lengo bila timeline, ni sawa na ndoto tu.” Lakini mimi naongeza kwamba “Lengo bila mikakati salama, ni sawa na ndoto tu”

Sasa ili Tanzania tuweze kufikia uchumi wa viwanda tunapaswa kufanya haya.

Nguvu kazi yenye uwezo wa kuendesha viwanda.

Director wa world Bank Tanzania Bella Bird hivi majuzi alisema… pamoja ya kuwa na nguvu kazi ya kutosha, bado asilimia zaidi ya 75 ya nguvu kazi ya Tanzania haina uwezo wa kuendesha uchumi wa viwanda.

Bella alisema uchumi wa viwanda utawezekana ikiwa, Tanzania itapunguza idadi hii ya wasio na uwezo mpaka ifikie asilimia angalau 51.

Elimu ya kujitegemea.

Hivi sasa uchumi una nafasi nyingi za kujiajiri kuliko kuajiriwa. Hivyo elimu inayotolewa ijenge uwezo kwa vijana wa kuwa wabunifu, kufanya kazi zaidi ya moja, na kuendana na kasi ya ukuwaji wa sayansi na teknolojia duniani.

Prof Humphrey Moshi muhadhiri wa uchumi chuo kikuu cha Dar es salaam ameiambia watupipo.com kwamba; serikali inapaswa Kuhakikisha Mitaala ya sasa inakuwa ya vitendo zaidi, kuliko kuchukulia jambo hili kisiasa.

Shule za Ufundi zirudishwe

Katika kumjengea uwezo zaidi kijana, kuna umuhimu mkubwa wa kurudisha shule za sekondary za ufundi, ambazo zilikuwa chini ya serikali. Mfano wa shule hizo ni shule ya secondary ya ufundi Ifunda Tech iliyoko mkoani iringa.

Lakini pia shule hizi ziwe katika kiwango cha kimataifa kwa upande wa teknolojia zinazotumika kufundishia.

Veta ya mwendokasi.

Mamlaka  ya elimu na ufundi stadi VETA, kwa sasa ndio mkombozi wa vijana wengi. Japo wengine hutoka huko wakiwa bado kabisa.

Veta inapaswa kuhakikisha ina uwezo wa kuchukua mhitimu wa darasa la saba, na kumfunda kwa kiwango cha kuweza kushindana, angalau katika soko la Afrika mashariki.

Elimu ya Kilimo

Nimekutana na vijana wengi wenye muamko wa kilimo ambacho ndio kinamiliki ajira zote za bure hivi sasa.

Tatizo ni kwamba vijana hawa hawana sehemu ya kujifunza kilimo biashara ambacho ndio mhimili mkubwa kwa viwanda.

Kukosa kwao uelewa wa kilimo bora wanaishia kupoteza muda wao na mitaji kisha wanarudi mitaani kulalamika.

Hivi sasa unaweza kukutana na kundi kubwa la wasomi lakini hawana ajira. Kila mmoja anasubiri nafasi itoke aajiriwe bila kujituma na kujiajiri.

Kama una lolote la kuongeza au maoni kuhusu article hii, andika comment yako hapa au tucheki watupipo.com Facebook au Twitter tupige stori zaidi.

Mwandishi: Macriner Watupipo

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com