Listen Live!

NI NANI ALIANZISHA THROWBACK THURSDAY?… Hivi ndivyo neno hili lilivyoanza kutumika.

Nani alianzisha throwback Thursday?

Mwanzo.

Neno Throwback linasekana kuanzia katika jamii African American, lilitumika kuunganisha matukio yaliyopita yanayoihusu jamii ya watu weusi popote walipo.

Hatua ya pili

Throwback lilionekana kwenye Urban Dictionary mwaka 2003, likitafsiriwa kwa maana ya kukumbushia kitu kilichopita zamani. Vintage or Classic.

Throwback Thursday

Mwanzoni mwa mwaka 2006 kwa mara ya kwanza lilionekana katika cartoon ya Retro… Iliyorudiwa kutengenezwa na Saxton Moore.

Moore alichapisha neno hilo kwenye blog yake.

Inasemekana kuwa, hii ndio mara ya kwanza kwa maneno haya kuunganishwa pamoja.

Kusambaa.

Matt Halfhill alihitaji kuingia kwenye biashara ya mtandao kwa kuanzisha Blog ya sneakers mwaka 2006. Aliyoiita nicekicks.com.

Baada ya kuona blogs nyingi zilikuwa na utaratibu wa kuwa na themed content kila wiki. Matt naye akaamua kutengeneza theme zake ili kufurahisha wasomaji wake.

July 2006 alianzisha theme mbili na kuziita “Release Reminder” kwa ajili ya kuzungumzia sneakers mpya ambazo zinakaribia kutoka, pamoja na “Throwback Thursday” kuzungumzia sneakers za zamani.

Hill anatajwa kuwa mtu wa kwanza kuyapa umaarufu zaidi maneno haya, ingawa baadhi ya machapisho yamemtaja kama mwanzilishi wa neno Throwback Thursday ambayo yameendelea kuwa trend, miaka zaidi ya 10 baadaye.

#TBT mpaka sasa imetumika zaidi ya mara 200 milioni kwenye mtandao wa Instagram pekee huku #ThrowbackThursday ikiwa imetumika mara 38 milioni kwenye mtandao wa Instagram.com

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com