SEHEMU 3 UTAKAZOPATA HAKI YAKO UNAPOVUNJA NDOA… Hii ndio namna ya kuondoa chuki baada ya kuvunja ndoa.

Siku hizi vijana wamekuwa wakifunga ndoa kwa wingi, na ndoa nyingi pia zimekuwa zikivunjika huku nyingi ni za vijana. Waswahili wanasema ujana ni maji ya moto… Je huu ujoto joto wa ujana ndio huzivunja ndoa?

Je ndoa zinapokatishwa, taratibu na sheria zinafuatwa ipasavyo? Jibu ni hapana, siku hizi za dotcom, wengi hufunga ndoa bila kufuata sheria na tamaduni, na wengi pia huvunja ndoa bila kufuata sheria.

Wakili Geofrey Shayo amezungumza na watupipo.com, kuniambia kuwa kutokufuata sheria, kumesababisha wanandoa kudhulumiana.

Wakili ametuambia haya ndio maeneo unapaswa kwenda kupata haki yako pindi unapovunja ndoa.

Taasisi za dini

Kuna ndoa za aina nyingi, Kikristo na za kiislamu, kama umefunga ndoa ya dini hakikisha unaimaliza pale ulipoifungia. Kama ni msikitini basi ruhusa ya kuvunja ipatikane msikitini na kama ni kanisani pia vivyo hivyo.

Peleka malalamiko yako kwenye mabaraza ya usuluhishi, mfano BAKWATA au KANISANI. Ndoa inavunjwa kufuata kanuni na taratibu, sio kukurupuka tu.

Baraza la usuluhishi la wilaya au kata.

Kama mlifunga ndoa kutumia taratibu za kiserekali basi wakati wa kuivunja sharti muende kwenye ofisi za serikali. Katika ofisi hizi huwa na mabaraza ya ndoa yaliyoteuliwa, kesi yako itasikilizwa na uamuzi utatolewa kufuata sheria na haki.

Endapo usuluhishi utashindwa kumaliza tofauti zenu. Mtatakiwa kwenda mahakamani.

Mahakama.

Katika kuwasilisha madai yako ya kuvunja ndoa, unatakiwa kuambatanisha cheti cha ndoa, na hati ya kutoka baraza la usuluhishi kuonesha kwamba malalamiko yameshindwa kutatuliwa na baraza hilo.

Kisha uamuzi utatolewa na mali mlizochuma zitagawanywa kutokana na ratio inayotakiwa.

Wakili Geofrey anasema, “endapo wanandoa watafuta taratibu hizi katika kuvunja ndoa, migogoro na chuki zinzofuata baada ya kuvunjika kwa ndoa zitapungua kwa kiasi kikubwa”

Lakini pia baadhi ya wanandoa wanasema; mambo haya ni magumu. Kuna mambo yanatokea katika ndoa ambayo husababisha migogoro hata kama sheria zikifuatwa.

Ndoa hazikuletwa ili zivunjike, kwa sababu ndoa ni muunganiko uluotukuka ambao unatarajiwa kuwa wa milele. Ndio maana sehemu ya kiapo cha ndoa husema “hadi kifo kitakapo tutenganisha” … hii ina maana kubwa.

Iliusikutane na masahibu ya kuvunja ndoa, hakikisha umeingia kwenye ndoa kwa sababu sahihi, wakati sahihi, na mtu sahihi ili matatizo yenu myamalize wenyewe.

Ukitaka kujua alama za kujua ikiwa unaoana na mtu sahihi au la. Endelea kufuatilia Stori zangu hapa watupipo.com na kama una lolote la kuongeza kwenye mada hii nicheki kupitia watupipo Facebook au Twitter

Mwandishi : Macriner Watupipo

Dar es salaam

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com