ASALI CHUNGU NI MOJA KATI YA AINA TATU ZA ASALI TANZANIA…Hivi ndio nyuki wanavyoitengeneza asali chungu.

Asali ni zao linalotokana na nyuki, na ni moja kati ya bidhaa ambayo inahitajika sana kutokana na faida zake katika afya ya mtumiaji.

Watu wengi tumekuwa tukiifanisha asali na vitu vitamu kutokana na utamu wake. Wapo ambao huwaita wapenzi wao “honey” wakiwa na maana ya asali na hata baadhi ya wazazi huita watoto wao honey.

Kazi za asali ni nyingi sana, lakini kwa ufupi tu asali inaweza kutumika kuponya majeraha, na pia kama dawa kwa wagonjwa ikichanganywa na vitu vingine.

Levina Swai ni mmoja wa wauzaji maarufu wa asali jijini Dar es salaam, ambaye anaeleza kuwa kuna aina mbalimbali za asali ikiwemo asali chungu.

Nimekusogezea aina hizi za asali ambazo unaweza kukutana nazo mtaani, usishituke.

Asali ya nyuki wadogo.

Kwa kawaida aina hii ya asali haina sukari kali, sukari yake ni ya kawaida mno. Aina hii ya asali inakuwa na ukakasi na mara nyingi huwa na rangi ya kahawia iliyokolea inayokaribia kuwa nyeusi.

Ambapo wagonjwa wa kisukari hushauriwa kuitumia maana huwasaidia kuhimili ugonjwa huo. Hata wagonjwa wa pressure nao hushauriwa kutumia aina hii ya asali.

Kwa nchi ya Tanzania aina hii ya asali hupatikana kwa wingi katika mkoa wa Tabora, Dodoma na Singida.

Asali ya Nyuki wakubwa.

Kwa kaiwaida aina hii ya asali huwa ni nzito kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha maji kulinganisha na asali ya nyuki wadogo. Huwa ni tamu kupitiliza na haina uchachu wa aina yoyote.

Hii huwa na rangi mbalimbali ikiwemo njano, nyeupe, kahawia iliyopoa na kahawia iliyokoza. Mara nyingi asali hii hutumika kulia na mikate kwa watu mbalimbali. Mara nyingi aina hii ya asali hupatikana mkoani Dodoma.

Asali Chungu

Asali hii ambayo pia hutengenezwa na nyuki wakubwa hupatikana kwa wingi katika mkoa wa Mtwara.

Asali hii pia utengenezwa na nyuki wakubwa ambayo pia ni dawa inayotibu magonjwa mengi ya mwilini ikiwemo magonjwa sugu. Asali chungu hii husabishwa na nyuki kufyonza miti michungu mfano Mwarobaini, Katani, Mdaa, Mkonga, Rovera na miti mingine mingi yenye asili ya uchungu.

Kwa muda mrefu wataalamu wamekuwa wakiishawishi jamii kutumia asali zaidi ya sukari. Hii ni kutokana na kutokuwa na side effects mwilini, na uwezo wake wa kulinda mwili au kuponya magonjwa mbalimbali.

Asante sana kwa kusoma article hii, kama unalolote ambalo unataka kufahamu kutoka kwenye bidhaa ya Asali nicheki kwenye watupipo Facebook au Twitter.

Writer: Baraka Ngofira Watupipo

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com