HATUA 4 MUHIMU ZA KULIPA MAHARI KWA SUKUMA TRIBE…Nyama hailiwi mpaka kieleweke!

Wasukuma ni  miongoni mwa kabila kubwa nchini Tanzania, kati ya kabila zaidi ya 120.

Kabila hili limeenea na kusambaaa katika mikoa ya Kanda ya ziwa, ambayo ni Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu na Tabora. Lakini pia kama ilivyo kwa makabila mengine wasukuma wamesambaa kila kona ya Tanzania.

Dhana ya mchumba na ndoa.

Zamani kulikuwa na dhana kwamba watu huenda kwenye sherehe au jando na kuchagua wachumba, lakini ukweli ni kwamba wazazi wana nafasi kubwa sana ya kupanga binti yao aolewe na mwanaume wa aina gani.

Sababu za mzazi kumchagulia binti yao mchumbi ni pamoja na magonjwa na mikosi, hivyo mwanaume huchunguzwa na wazazi wa mwanamke.

Watu pipo inakutana na doto kuhenga ambaye anatokea katika familia ya kichifu ya kabila la wasukuma anaeleza hatua ambazo mwanaume anapaswa kuchukua akitaka kuoa binti wa kisukuma

Nitanilo

Hili ni neno la kisukuma lenye maana kuitwa au kuitana. Katika hatua hii kijana anayetaka kuoa hutuma mzee au wazee kwa familia ya yule binti, na akifika katika ile nyumba wazazi wa binti humuita shangazi, na baadae shangazi humuita binti na kumweleza kuhusu ujio ule.

Kupanga

Hilo ni neno la kisukuma na kiswahili na lina maana sawa na kiswahili kupanga.

Stage hii wazee wa pande zote mbili hukutana kujadililiana kuhusiana na mahari, ambayo inatakiwa ili kumuoza binti na baada ya pande zote mbili kukubaliana, mahari hutolewa.

Doto Kuhenga (UDSM) kijana kutoka familia ya ki-chief ya katika kabila hilo, ameiambia watupipo.com kwamba “hiyo ndio sehemu ngumu zaidi katika mchakato wa kuoa usukumani”

Wakati majadiliano yakiendelea, wazee hupewa chakula cha kawaida kwa mila za kisukuma, ambapo chakula hicho ni ugali na majani ya kunde yaliyokaushwa kwa kisukuma wanaita mkarambo.

Nyama hailiwi kwa muda huu mpaka makubaliano yafikiwe, then wakina mama huitwa kupiga vigelegele na mbuzi huchinjwa tayar kwa kujinoma.

Wanawake hawahusishwi katika majadiliano ya mahari.

Tarehe ya kulipa mahali

Mahari mara nyingi huwa ni Ng’ombe au vitu vingine. baada ya kukubaliana tarehe ya kulipa hupangwa.

Mahari hulipwa kuanzia mwezi mmoja au miezi mitatu baada ya makubaliano.

Sherehe

Baada kulipa mahali hatua inayofuata ni sherehe. Mara nyingi kwa wasukuma sherehe hufanywa upande wa mwanamke, kutokana na mwanaume ndio huenda kuchukua mke wake.

Asante kwa kusoma article yangu, kama una lolote la kuongeza kwenye sheria hizi za mahari ya kabila la kisukuma nicheki kupitia watupipo.com Facebook au Twitter… Cheki hapa kujua jinsi ya kuvunja ndoa na kupata haki yako.

 

Writer : Macriner Watupipo

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com