Imagine unahudhuria harusi uliyopendeza zaidi ya bi harusi!

Wasimamizi wa harusi ni watu muhimu katika siku hiyo kubwa maishani. Wasimamizi wa harusi wanahitaji kupendeza na kuipa hadhi sherehe nzima. Doreen Mmary ni mmoja wa wapambaji wa maharusi maarufu maeneo ya Mwenge anaelezea mambo muhimu ya kuzingatia pale Bridesmaid anapotaka kuchagua gauni la harusi.

Yafuatayo ni mambo muhimu 5 ya kuzingatia pale unapochagua gauni la kuvaa siku hiyo.

Epuka kuwa kichekesho

Unapochaguliwa kuwa msimamizi wa harusi jaribu kuchagua gauni ambalo litakufanya uonekane vizuri na si kugeuka kuwa kichekesho. Unashauriwa ufikirie nje ya box maana ni vyema kuwa tofauti lakini usiwe kichekesho.

Chagua mshono simple.

Ni vyema kuchagua mshono simple ili kulifanya gauni la bibi harusi na msimamizi wa harusi lionekane vyema. Pia unapochagua mshono simple inapunguza gharama zisizo za msingi katika kitambaa na mashono.

Unashauriwa kushona vitambaa vya Santeen

Vitambaa vya sateen vinapendeza kushona magauni ya wasimamizi wa wa harusi kwa kuwa hung’ara na kuonyesha vizuri mshono  wa gauni. Lakini pia unakufanya msimamizi wa harusi kuonekana vizuri yaaani upendeze.

Chagua rangi inayoendana na tukio lenyewe

Uchaguzi wa rangi nao ni muhimu, maana ni mara chache maharusi huchagua wasimamizi wavae gauni gauni jeusi hasa kutokana na maana ya rangi hiyo kuakisi upendo na amani. Lakini wasimamizi wengi ushauriwa kuchagua rangi nyekundu, damu ya mzee, nyeupe, Aquatic green, purple na nyingine.

Changanya vitambaa

Wasimamizi wa harusi hushauriwa kushona mtindo ya kuchanganya vitambaa kwenye magauni yao, hii inapendezesha magauni yao. Lakini hapa tahadhari inatolewa vitambaa vinavyochanganywa vingi hadi vikakera.

Asante kwa kusoma article hii, kama una lolote la kungeza hapa tafadhali niwekee kwenye Comments au niwekee kwenye Facebook au Twitter

 

Writer: Baraka Ngofira Watupipo

 

You may also like...

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com