UNATAKA UTAJIRI?… Lazima ukubali kufuata masharti haya muhimu.

Vijana wanatamani kuwa matajiri asubuhi na mapema, lakini wengi hawajui namna gani watakuwa matajiri, na hapa ndipo Ile ndoto ya utajiri inapokuja na kuamua wajikuta masikini.

Kama kijana wa kisasa  na unatamani kuwa tajiri katika umri mdogo ni lazima kufanya haya.

Photo unknown

Save pesa na wekeza ukiwa kijana

Kwa mujibu wa mshauri wa biashara William Bernstein’s toka nchini Marekani anasema kijana anashauriwa ku-save kiasi cha mshahara katika akaunti ya akiba, ili kumsaidia katika uanzishaji wa  wazo la biashara ambalo litamletea faida kubwa.

Anashauri kuweka akiba angalau kwa miaka mitatu au kwa kipindi ambacho unaweza kuanzisha wazo lako la biashara.

Fikiria zaidi kuhusu kutengeneza pesa

Unaweza ukawa unawekeza lakini mawazo yako yasijikite zaidi katika kutafuta pesa.

Benjamin Ferdanandes mtaalamu wa biashara na fedha toka Tanzania wakati akizungumza na watupipo.com anashauri vijana kutumia muda mwingi katika kufanya kazi za kuingiza pesa na sio mambo mengine.

Jifunze zaidi kuhusu udhibiti wa pesa

Anne Scorgie katika kitabu cha Well-Heeled The Smart Girl’s Guide to Getting Rich anasema kupata utajiri sio bahati, ila ni kuwa na uhuru wa kipesa  na kufikia malengo.

Scorgie anashauri kuzingatia sana matumizi ya pesa, kwani matumizi mabaya ya pesa yanaweza kufanya usifikie ndoto zako, na kuweza kukushusha chini kiuchumi kuliko ilivyokuwa awali.

Jifunze kwa waliofanikiwa

Kutafuta pesa na kuzimiliki ni kitu ambacho unapaswa kujifunza na walimu wakuu watu waliofanikiwa kuzitafuta na kuzimiliki pesa.

Mara nyingi vijana hawajiweki kwenye mazingira ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa. Benjamin Fernandes anasema mafanikio hayaji toka mahali kusikojulikana bali ni kutokana kujifunza kwa walioweza na lakini ni lazima kuwa na utayari.

Kukubali changamoto

Changamoto zimewafanya wengi kukata tamaa na kushindwa kuendelea na mipango ambayo wamejipangia. Ferdanandes anasema ili kufikia malengo ya utajiri, misukosuko ni lazima itokee ili kukujenga kwani hakuna biashara isiyokuwa na changamoto.

Vijana ndio nguvu kazi kubwa ya taifa lolote lile duniani kiuchumi na ili kijana aweze kuwa bora ni lazima vijana kufanya kazi kwa bidii.

Asante kusoma article hii, kama una chochote cha kuongezea au una mada ungependa niiandike please cheki na mimi kupitia kwa kuandika comment yako hapo chini au Facebook na Twitter.

 

Writer: Mackrina watupipo

Tanzania

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com