MAMBO 2 YATAKAYO KUKAMILISHIA MALENGO YAKO KILA MWAKA… Kula haraka sio kutangulia kushiba.

Kila mwaka unapoanza mood ya watu hubadilika huku wengi wakiwa na matarajio makubwa. Wengi huwa tunaamini kwamba huu ndio mwaka wetu wa kufanikiwa. Lakini wengi huwa wanasahau kabisa mipango yao kabla hata mwaka haujaisha.

Hii inaweza kukufanya ukakata tamaa kabisa na kujiona pengine hauwezi kufanikisha chochote kwenye maisha yako.

Viko vitu kadhaa vinavyosababisha wengi washindwe kufanikisha mipango yako, na hapa nitazungumzia viwili ambavyo ni tabia yako na aina ya malengo unayoweka.

Tabia.

Kila mtu ana tabia zake, na mara nyingi kuna utofauti kubwa kutokana na mazingira na jamii unayoishi nayo. Lakini pia kila lengo unalojiwekea lina mbinu zake za kulifikia.

Tabia zako zinaweza kufanikisha au kufelisha malengo yako, kwa mfano; Ukiwa unataka kupunguza uzito au unene unapaswa kufanya mazoezi na kuwa na utaratibu mzuri wa kula vyakula vitakavyokusaidia kufikia lengo lako.

Hii itakufanya uache kula baadhi ya vitu ambavyo pengine umezoea kula mfano chips mayai, burgers, pizza na vingine. Je uko tayari kubadilisha tabia yao na kufuata mpango mzuri wa kula? Je uko tayari kufanya mazoezi ipasavyo?

Ili kuweza kufanikiwa katika kubadilisha tabia na habits zako, unashauriwa kuanza kitu kidogo kidogo. Mfano unataka kuanza kuacha kula chips mayai… usianze kwa kusema kuanzia leo hautakula kabisa chips mayai, bali uanze kwa kupunguza idadi ya siku unazokula.

Kama ulizoea kula chips mayai kila siku..

Unaweza ukaanza kwa kusema “sitakula chips mayai siku za weekend tu kwanza” nenda na utaratibu huu mpaka utakapouzoea na kuona ni kawaida kutokula chips weekend, sasa ndio unaweza kuongeza siku zingine mpaka ufikie lengo.

Tabia inaweza kubadilishwa kwa kuanza kubadilisha mazoea. Na mazoea yanabadilishwa kwa utaratibu.

Vunja Malengo yako vipande

Unapojiwekea malengo, mfano malengo ya kujenga nyumba. Unatakiwa uligawe lengo hilo kwenye vipengele na process zinazohitajika kukamilisha nyumba.

Ujikite kwenye kugawa kila process na uangalie namna ya kukamilisha vitu vidogo vidogo. Mfano utahitaji kiwanja, je kiwanja utakipata wapi? Pesa za kiwanja utazipata wapi?

Utahitaji matofali, je utayatoa wapi? Cement kiasi fulani je utatoa wapi pesa ya kununulia? Hakikisha kila kitu umekiweka kwenye mfumo wa mchakato ili unaposema nyumba, uone vitu vidogo vidogo vitakavyoijenga.

Hii itakusaidia sana kujua kwamba lengo lako linafaa kukamilika mwaka huu au linahitaji miaka miwili au linahitaji miezi sita.

Hii pia itakusaidia usipoteze dira katikati ya mwaka baada ya kuona process ya kujenga nyumba ni ngumu zaidi ya ulivyofikiria.

Kuna mengi unaweza kufanya ndani ya mwaka mmoja katika kutimiza malengo yako, ila kwa sasa niandikie maoni yako kuhusu article hii. Pia nicheki Facebook au Twitter

 

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com