KENYA IKIENDELEA HIVI, TANZANIA ITAONGOZA KIUCHUMI EAST AFRICA.

Kenya na Tanzania ndio nchi zenye uchumi mkubwa zaidi katika ukanda wa Africa mashariki, Tanzania ikiwa na GDP ya $47.4 billions huku Kenya ikiongoza kwa GDP ya $68 billions mwaka 2016. Nchi zote zinatarajia ongezeko mwaka huu lakini Tanzania inatarajia kuongezeka kwa kasi zaidi ya Kenya.

Tukiachana na historia za kale ambapo Tanzania ilikuwa na uchumi mkubwa zaidi kuliko Kenya 1982 then Kenya ikachukua nafasi ya kwanza 1984 baadae Tanzania ikaongoza tena, then 1987 Kenya ikachukua ukuu moja kwa moja mpaka sasa. Tanzania kwa miaka 20 iliyopita imekuwa ikifukia Gap lililoko kati ya uchumi wake na Kenya.

Uchumi wa Tanzania kwa miaka mingi umekuwa ukiongezeka kwa zaidi ya asilimia 7, huku Kenya umekuwa kwa asilimia 5 mfululizo, hii inamaanisha kwamba, endapo trend itakwenda hivi kwa nchi hizi huenda Tanzania ikachukua ukuu wa uchumi kwenye ukanda wa Africa mashariki ndani ya miaka 10 ijayo.

Hizi ni sababu kuu ambazo zinaweza kufanya uchumi wa Tanzania kuongoza Africa mashariki.

Soko kubwa

Tanzania inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya million 55 huku Kenya ikiwa na population ya 49 million, hii inamaanisha kuna soko kubwa zaidi la bidhaa za ndani Tanzania zaidi ya lililoko Kenya.

Siasa na usalama

Kenya kwa miaka ya karibuni imekuwa na changamoto za kiusalama ukilinganisha na Tanzania. Mfano ni uchaguzi wa mwaka 2017 ambao umekuwa na tension kubwa baada ya supreme court of Kenya kufuta matokeo na kuamuru uchaguzi mpya ufanyike.

Hii imeongeza tension mtaani na wafanyabiashara ndogondogo na wale wa kati mpaka wakubwa wamekumbwa na challenge kubwa kutokana na upungufu wa mzunguko wa pesa.

Lakini pia Kenya imekuwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa kundi la Somalia la Al-shabaab, pamoja na chaos zilizozuka mwaka 2008, ambazo zilitingisha uchumi wa Kenya.

Rasilimali za mafuta na gesi.

Pamoja na kwamba nchi zote mbili zimegundua kuwwepo kwa mafuta, Tanzania imegundulika kuwepo kwa kiwango kikubwa cha helium gas ambayo ni rare na expensive zaidi duniani.

Punguzo la imports

Tanzania imepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa bidhaa kutoka Kenya kwa asilimia 34 kufikia $ 77 milioni mwaka 2016. Hapo awali Tanzania ilikuwa moja kati ya nchi zinazonunua bidhaa nyingi kutoka Kenya.

Punguzo hili linatokana na ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa za ndani, pamoja na expansion ya bandari ambapo bidhaa zilizokuwa zinaagizwa na Kenya kisha kuuzwa Tanzania zimekuwa zikiagizwa moja kwa moja kupitia bandari ya Dar es salaam.

Real estate and transportation

Hivi karibuni Dar imekuwa ikifanya mageuzi ya kiuchumi ikiwemo system ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi BRT ambayo imezinduliwa mwaka 2016 na kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza shida ya usafiri jijini Dar.

Kama ilivyo kwa mafanikio ya reli ya standard gauge iliyozinduliwa mwaka 2017 Kenya, nchini Tanzania pia ujenzi wa reli aina hii umeanza.

Katika ripoti ya world bank cities report ya February 2017, imeonesha real estate ya Dar ikiwa mbele ya Nairobi. Dar real estate iko na value ya $12 billion huku Nairobi ikiwa na $9 billion.

Ingawa Worldbank imeonesha kwamba itachukua muda mrefu sana kabla ya Tanzania kuongoza kiuchumi Afrika mashariki zaidi ya inavyoonekana.

Tofauti kubwa ninayoiona kati ya nchi hizi mbili ambayo inaweza kuwa na direct impact kwenye uchumi ni sekta binafsi. Sekta binafsi Kenya imekuwa mbele kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi na hata baadhi ya kampuni kubwa ziko na matawi Tanzania. Mfano KCB, Sportpesa nk.

Ni rahisi zaidi kuanzisha biashara ndogondogo Kenya zaidi ya Tanzania, hasa katika suala la urasimishaji na huduma za kiserekali. Sio rahisi kusajili biashara ya chakula au dawa Tanzania na ndio maana wajasiriamali wadogo hufeli.

Huu ndio msimamo wa uchumi kwa nchi rasmi Afrika mashariki.

   Country                                    Population                                    GDP

  1. Kenya                                     49 million                                      $68 billion
  2. Tanzania                               55 million                                      $47.4 billion
  3. Uganda                                 41 million                                      $26 billion
  4. Rwanda                                11 million                                      $8 billion
  5. Burundi                                10 million                                      $3 billion

Asante kwa kusoma article yangu hapa watupipo.com kama una chochote cha kuongeza kuhusu uchumi wa Afrika mashariki niandikie kwa email watupipo.com@gmail.com au Facebook na Twitter

Writer: Abdulkweli

You may also like...

WP Facebook Auto Publish Powered By : XYZScripts.com